Latest Updates

NEWS - Serikali yasisitiza dhamira yake kuhusu ndoa za utotoni

11:52 AM

August 19 2016 Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto amefanya uzinduzi wa mradi wa kukusanya nguvu za pamoja kulinda haki za wasichana nchini Tanzania awamu ya II jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Mwalimu amesisitiza dhamira ya Serikali ni kuendeleza jitihada za kufanya marekebisho ya sheria ya ndoa ya mwaka 1997, hususan katika kifungu 13 (1) cha sheria ya ndoa kinachoeleza kuwa umri wa mtoto wa kike kuolewa ni kuanzia miaka 15.

Aidha Waziri Mwalimu ametoa ufafanuzi zaidi kuhusu Serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu kuhusu sheria hiyo kuwa ni ili kupata maamuzi ya juu zaidi ambayo hayataweza kupingwa na mahakama nyingine ya chini.

NEWS - VIPENGELE TUNZO ZA EATV AWARDS VIKO HAPA

11:45 AM

Vipengele vya tuzo mpya zilizoanzishwa na kituo cha runinga cha East Africa Televisheni, EATV Awards, vimetangazwa Ijumaa hii.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Mkuu wa masoko wa kituo EATV,Roy Mbowe alisema tuzo hizo zitakuwa na vipengele 10 zitakazohusisha muziki, filamu na tuzo moja ya heshima.
Vipengele hivyo ni:

1. Mwanamuziki bora wa kiume
2. Mwanamuziki bora wa kike
3. Mwanamuziki bora chipukizi
4. Kundi bora la muziki
5. Video bora ya muziki
6. Wimbo bora wa mwaka
7. Muigizaji bora wa kiume
8. Muigizaji bora wa kike
9. Filamu bora ya mwaka
10. Tuzo ya heshima itakayotolewa kwa mtu au kampuni iliyochangia kwa kiasi kikubwa katika kazi za muziki.

Mbowe amesema kazi za sanaa zitakazoruhusiwa kuingia kwenye vipengele ni zile zilizotoka kuanzia Julai 1 2015 – 30 Juni 2016. Tofauti na tuzo zingine, wasanii wanaotaka kushiriki watalazimika kujaza fomu za kutaka kutajwa kwenye tuzo na kuwasilisha kazi husika ambapo mchakato wa uchambuzi wa kazi hizo utachukua kipindi cha mwezi mmoja kabla ya majina yaliyoingia kwenye tuzo hizo kutajwa na kuanza kupigiwa kura.

Hata hivyo amedai kuwa pamoja na wananchi kupiga kura, kutakuwepo na jopo la majaji litakaloshiriki kupata washindi. Tuzo hizo zinazodhaminiwa na kampuni ya Vodacom, zitatolewa December 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

RAZA LEE KUMALIZANA NA TAIFA YA JANGOMBE JUMAMOSI SAA 3 ASUBUHI, APANIA KUINUNUA KWA SHS MILIONI 35

7:12 AM

Mohd Ibrahim “Raza Lee” siku ya Jumamosi ya tarehe 30 July anatarajia kuinunua timu ya Taifa ya Jangombe kwa shs Milioni 35.

Leo Usiku atafunguka LIVE kupitia kituo cha Radio cha Coconut FM 88.9 kwenye kipindi chao cha Coco Sports kuanzia saa 2:00 za usiku.

TETESI ZA SOKA ZANZIBAR LEO JULY 28, 2016

7:07 AM

Adeyum Saleh afagiliwa usajili wake wa kwenda Stand United, Wakala wa Mchezaji mpya wa Stand United Saleh Machupa ambae pia ni baba mzazi wa mchezaji huyo amesema mtoto wake amekwenda timu sahihi na yeye ndio aliemshauri kwenda timu hiyo baada ya kuondoka Coast Union ya Tanga ilioteremka daraja.

Mlinda mlango wa zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Suleiman Hamad ambae kwasasa anacheza timu ya Kijichi anatarajiwa kuondoka klabuni hapo na kujiunga na moja ya timu ya Ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwemo Mtibwa Sugar , wakati huo huo pia huwenda akarejea timu yake ya Zamani ya Black Sailors.

Timu ya Small Renger inayoshiriki ligi daraja la pili Wilaya ya Mjini ipo mbioni kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani Hafidh Ali “Mess wa Makadara” kwa gharama yoyote kutokea klabu yake ya sasa ya Muembe ladu.

Yahya Haji “karoa” mshambuliaji wa Villa United “Mpira Pesa” anawindwa na timu ya KVZ na JKU, mchezaji huyo amezisaidia kuzipa ubingwa wa Rolling Stone timu ya Mjini Zanzibar na Villa United Daraja la Pili Wilaya ya Mjini.

Mashabiki wa Soka Visiwani Zanzibar wameipa tano timu ya Kombain ya Mjini Zanzibar baada ya kuonesha soka safi katika mchezo wa kirafiki uliosukumwa jana usiku kwenye uwanja wa Amaan ambapo timu hiyo imepigwa 1-0 na Azam FC.

Mohd Ibrahim “Raza Lee” siku ya Jumamosi ya tarehe 30 July anatarajia kuinunua timu ya Taifa ya Jangombe kwa shs Milioni 35. Leo Usiku atafunguka LIVE kupitia kituo cha Radio cha Coconut FM 88.9 kwenye kipindi chao cha Coco Sports kuanzia saa 2:00 za usiku.

Utafiti- Unajua watu walefu zaidi wanapatikana wapi?

7:28 AM

Utafiti mpya umeonesha kwamba wanaume wa Uholanzi ndio warefu zaidi duniani, na upande wa wanawake, wanawake wa Latvia ndio warefu zaidi.

Kimo cha wastani kwa wanaume Uholanzi ni futi 6 kwa sasa (sentimeta 183), na kimo cha wastani kwa wanawake wa Latvia ni futi 5 inchi 7 (sentimeta 170).

Utafiti huo, ambao matokeo yake yamechapishwa kwenye jarida la eLife, umefuatilia kimo cha watu na mabadiliko yaliyotokea katika mataifa 187 tangu 1914.

Utafiti huo umebaini kwamba wanaume wa Iran na wanawake wa Korea Kusini ndio walioongeza kimo zaidi, wakiongeza kimo cha wastani kwa zaidi ya inchi 6 (sentimeta 16) na inchi 8 (sentimeta 20) mtawalia.

Wanawake wafupi zaidi duniani wanapatikana nchini Guatemala huku wanaume wafupi wakitokea Timor Mashariki.

Mwanamke wa umri wa miaka 18 kwa wastani nchini Guatemala alikuwa na kimo cha futi 4 inchi 7 (sentimeta 140) mwaka 1914 utafiti wa kwanza ulipofanywa na sasa kiwango hicho hakijafika kabisa futi 4 inchi 11 (sentimeta 150).

Kimo cha wastani kwa wanaume Timor Mashariki ni futi 5 inchi 3 (sentimeta 160).

Watafiti hao wanasema kuwa chembe chembe za jeni hubadilikabadilika, lakini cha muhimu zaidi ni kuwepo kwa lishe bora, usafi na matibabu ya hali ya juu.

Mataifa yenye wanaume warefu zaidi duniani 2014 (kwenye mabano ni nafasi iliyoshikiliwa 1914):

Uholanzi (12)
Ubelgiji (33)
Estonia (4)
Latvia (13)
Denmark (9)
Bosnia na Herzegovina (19)
Croatia (22)
Serbia (30)
Iceland (6)
Jamhuri ya Czech (24)

Mataifa yenye wanawake warefu zaidi duniani 2014 (kwenye mabano ni nafasi iliyoshikiliwa 1914):

Latvia (28)
Uholanzi (38)
Estonia (16)
Jamhuri ya Czech (69)
Serbia (93)
Slovakia (26)
Denmark (11)
Lithuania (41)
Belarus (42)
Ukraine (43)

News- bila wivu hakuna mapenzi jux

10:26 AM

Msanii Jux ambaye sasa ni mpenzi wa Vanessa Mdee amefunguka na kusema kuwa wimbo wake mpya 'Wivu' ambao unafanya vizuri kwa sasa hajaimba kwa ajili ya mpenzi wake Vanessa Mdee.

bali ameimba wimbo huo kutokana na hisia kwani jambo hilo linawakuta wengi ambao wanapendana kweli katika mahusiano yao ya kila siku.

Jux akizungumza kwenye kipindi cha ENEWZ ya EATV alidai kwenye mapenzi kama hakuna wivu kati ya wawili wapendanao hapo kunakuwa hakuna mapenzi ya kweli kati yao kwani wivu ndiyo ishara ya upendo wa kweli.

"Wimbo wa Wivu ni matukio ya kimapenzi ambayo yanatokea kwa watu wengi ila siyo kama nimejiimbia mimi, unajua kabla sijarekodi wimbo ule tukiwa studio niliwauliza wakina Bob Manecky na wengine jamanii mnadhani 'idea' hii inaweza kuwa sawa ndipo hapo wakaniambia ni wazo zuri kwani kwenye mapenzi bila uwepo wa wivu kuna kuwa hakuna mapenzi ya kweli, ndiyo hapo nikajua kumbe suala hili linawagusa watu wengi" alisema Jux.

Mbali na hilo Jux amesema kuwa hivi sasa muzuki unakuwa kama haupo kutokana na ukweli kwamba watu wanatanguliza life style mbele kuliko hata kazi zao na ndiyo maana wasanii wengi wakitaka kutoa kazi zao wanafanya mambo mbalimbali kutafuta kiki ili waweze kutambulisha kazi zao hizo.

"Sipendi sana kuulizwa maswali juu ya Vanessa napenda niulizwe maswali juu ya kazi zangu mimi kama msanii, ili nitangaze kazi zangu mimi ndiyo maana kuna vitu saizi sisi tunavikwepa kwa makusudi, tunataka kurudisha muziki hivyo mambo ya kiki, life style tunataka yakae pembeni" alisema Jux

NEWS- watakao sambaza Ky kukiona

4:17 AM

MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambayo yatabainika  yanaendelea   kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, yatafutiwa usajili.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa ‘facebook’.

Alisisitiza kuwa serikali italisimamia suala hilo kwa ukamilifu.

“Sijapiga marufuku matumizi ya vilainishi, ukweli nimepiga marufuku mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kununua na kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanaume wenzao na sababu nimeshazieleza,” aliandika na kuongeza:

“Na nafurahi kuwajulisha kuwa tayari baadhi ya mashirika hayo yameanza kutekeleza agizo hili kwa   kuondoa vilainishi kwenye miradi yao. Nayapongeza sana. Niendelee kuyataka mashirika mengine kutii agizo hili ambalo tutalisimamia kwa ukamilifu.

“Serikali haitasita kuchukua hatua ikiwamo kuyafutia usajili mashirika yanayoendelea na miradi ya kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja”.

Aliyataka mashirika hayo kushirikiana na serikali kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kujikita kwenye afya nyingine  inayozingatia sheria za nchi  na mila na desturi za Watanzania.

Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, Waziri Ummy alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini matumizi ya vilainishi hivyo yanachochea kuongezeka  vitendo vya ushoga ambavyo ni kinyume na sheria za nchi.

“Lengo pia ni kudhibiti maambukizi ya VVU kwa sababu katika   wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, asilimia 23 tayari wana maambukizi hayo.

“Tumebaini baadhi ya wadau wanaotekelezeka shughuli za makundi maalum wamekuwa wakikiuka taratibu za  utendaji na kusambaza vilainishi hivyo.

Awali agizo hilo lilizua mjadala mkubwa katika mitandao ya  jamii, wengi wakikosoa uamuzi huo wa Serikali kupiga marufuku vilainishi hivyo.

Walisema  kwamba vinatumika katika mambo mengine mtambuka hususan hospitalini huku wengine wakisema viendo vya ushoga havichangiwi na kuwapo   vilanishi bali ni mmomonyoko wa maadili uliotamalaki nchini

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates