Mama Mzazi wa wasanii wakongwe wa muziki wa
kizazi kipya, Professa Jay na pia Black Rhino, marehemu Bi Rosemary
Majanjara anatarajiwa kuzikwa Jumapili hii katika makaburi ya Kinondoni
jijini Dar es Salaam.
Taratibu za msiba wa mama huyu, zitaanzia asubuhi nyumbani kwa
Professa Jay Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam kwa sala, na pia kutoa
heshima za mwisho na kisha kuelekea makaburini katika maeneo ya maziko.
Wadau ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa staa wa rap hapa Bongo,
Professa Jay, pamoja na ndugu yake Black Rhino, wameendelea kujitokeza
kutoa pole pamoja na kushiriki kwa nafasi zao katika msiba mkubwa wa
Mama Mzazi wa wasanii hawa ambao upo Mbezi jijini Dar es Salaam.
chiwileinc inaendelea kuwatakia wasanii hawa nguvu katika kipindi hiki
kigumu, na Mungu ailaze roho ya amarehemu mahala pema peponi Aamin.
No comments:
Post a Comment