Congrats to Nicholaus Haule a.k.a Black Rhino and Beatrice Mbaga Haule on Your Wedding Day




    
Ni zaidi ya miaka kama 8 hivi toka niwaone mkiwa wote Black Rhino & Beatrice, sasa ile ndoto yenu imekamilika jumamosi hii iliyopita ya tarehe 1. Mungu awabariki muendelee kuwa pamoja hivyo hivyo mpaka kifo kitakapo kuja kuwatenganisha ndugu zangu. Na mimi nawaahidi kufuata nyayo zenu, ingawa sikuwepo katika sherehe yenu kwa kuumwa basi naimani moyo wangu upo nanyi siku zote.


Ndoa yao imefungwa jana kwenye kanisa la St. Joseph jijini Dar es Salaam ambapo Rhyno na mke wake walianzisha uhusiano miaka saba iliyopita na kuishi pamoja kwa miaka mitatu kabla ya kufunga ndoa.

Kaka yake Profesa Jay ni miongoni mwa watu waliouhudhuria katika harusi hiyo na kuwaburudisha kwa kwa show kali ya wimbo wake unaotamba kwa sasa, ‘Kamiligado.

Black Rhyno naye alikiacha kiti cha Bwana Harusi na kutumbuiza kwenye sherehe hiyo.

Mastaa waliohudhuria kwenye harusi yake ni pamoja Sharo Milionnare, Soprano, Rashida Wanjara na wengine.

Msanii huyo amesema pamoja na kufunga ndoa bado ataendelea kufanya muziki na kuendelea na kazi katika benki ya Barclays aliyopo sasa.



“Sioni kama kuna chochote kinachoweza kubadilika katika maisha yangu mimi kwa kile ambacho mimi nakitaka kwasababu siku zote mimi huwa ni mtu ambaye niko focused na ninaanalyse kuona kwamba kitu gani naweza kukifanya kwa time gani, sidhani kama kutakuwa na kitu kinaweza kubadilika ama kuaffectiwa  kwa namna yoyote ile.”

Ameongeza kwa kuwashauri wasanii wenzake ambao bado hawajaoa kuwa focused, makini nakuwa na plan katika maisha yao na sio kuishi tu bila kujua kesho itakuaje.

“Wakishakua na plan kwenye maisha yao definitely, ni rahisi kwao kuweza kumuomba Mungu ampatie mtu ambaye anaweza akamfaa katika maisha yake kwasababu kuoa si kitu ambacho mtu unaweza ukaiga kama fashion kwamba Rhyno ameoa basi na mimi nikaoe. Ni kitu ambacho kwanza lazima uwe umejitayarisha. Ni kitu ambacho lazima uwe na plan nacho, ni kitu ambacho kinatakiwa kianze kwenye nafsi yako uwe umetaka  kufanya kwa kuona kwamba umekuwa tayari  unahitaji kukifanya kwasababu tayari umeshampata mtu anayekufaa, Mungu amekupatia na hauna sababu yoyote ya kuendelea kusubiri.Kwahivyo, mimi nachoomba ni kwamba, watu wawe focused, wawe makini kuplan maisha yao, mapema sio tu unaishi huelewi kesho itakuaje."

Kuhusu mpango wa Profesa Jay naye kufunga ndoa amesema ana mpango huo tangu siku nyingi, japo bado hajampata mtu anayefaa kuwa mke wake.

chwileinc inamtakia maisha Black Rhyno na mke wake Beatrice maisha mema ya ndoa.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates