
.
Baada
ya stori kuandikwa kwenye magazeti kwamba Staa Diamond Platnums
anadaiwa kumtelekeza baba yake na hamjali wala hataki kusikia stori
zake, hii ndio kauli ya Diamond kuhusu hiyo ishu.
Amesema
“kiukweli ni vitu ambavyo mimi vimenishangaza sana kwa sababu sijui
chochote nakuja kukuta tu kwenye magazeti, na nisingependa nisikie
swala la mzazi wangu kusema mimi ni mtoto wake sijui nini na nini
kwamba mimi nafanya starehe sihusiki na yeye sio kauli nzuri kiukweli,
ina maana ananijua kwamba mimi ni mwanae baada ya kuwa DIAMOND”
Kwenye
line nyingine Diamond amesema “siku zote kama alijua mimi ni mtoto
wake basi angenisomesha na kunipa elimu nzuri lakini siku zote
nilihangaika na Mama yangu mzazi akanikuza na kunisomesha kwa shida na
tabu zote mpaka leo nimekua hivi, nisingependa kumsikia mtu yeyote
anaongea kwamba mimi ni mtoto wake au yeye ni nani kwa sababu siku zote
hawakuonekana, wasitake kuonekana kipindi cha Maslahi mtu ndio
anajifanya anahusika sana na mimi kama mtoto wake”
“Haya
mambo nilianza kuyasema toka natoa single ya binaadam sikujua hata
kama leo ningekuja kuwa na Prado, makazi au kuwa na haya mafanikio
mengine, baba yangu ataendelea kuwa baba yangu tu ila siwezi kumpa
kipaumbele kama ninachompa mama yangu kwa sababu kama angetaka hilo
angenijali toka mapema” – DIAMOND.
Post a Comment