MwanaFA akerwa na makampuni ya simu kugeuza nyimbo kuwa matangazo

mwana fa

Rapper Hamis Mwinjuma aka MwanaFA ameelezea kukerwa na mtindo uliopo sasa wa makampuni ya simu kugeuza nyimbo za wasanii kuwa matangazo na kuelezea kuwa ni ufinyu wa ubunifu.
“Ndugu makampuni ya simu,mashindano ya kubadili nyimbo za bongo fleva kuwa matangazo yenu yametosha sasa!fanyeni kubuni kitu kipya,ahsanteni!” ametweet leo.
MwanaFA siye pekee aliyechukizwa na kitendo hicho kilichokithiri kwa makampuni ya simu nchini.
Mtangazaji na mbunifu wa vipindi na masuala mbalimbali wa Clouds Fm Cindy naye pia ameonesha kusikitishwa na tabia hiyo.
"Salaam kwa kampuni zetu za simu, matangazo bila kutumia nyimbo na wasanii wa muziki yanawezekana kwa kuajiri ubunifu 'kidogo tu' katika utunzi wenu wa matangazo na njia za mawasiliano kwa jamii!!ni hayo tu,” aliandika kupitia Facebook.
“Inachosha kila mara kusikia nyimbo zetu zote nzuri zimebadilishwa kuwa na ujumbe wa tangazo... Mbaya zaidi ni kuona kampuni zinavyoigana kana kwamba hiyo ndio namna pekee ya kutangaza bidhaa/huduma zao...inanionyesha pia ufinyu wa ubunifu wao katika utoaji wa huduma zao!!!”
Aliongeza,If only zingekuwa ni original production and not the renditions of popular songs/artists performances...then that would be a step towards creativity in all this. Atleast get a vocalist, write an original music (creatively) n produce AN ORIGINAL musical ad with FRESH melodies...but NOT get a popular (over played) song, change lyrics (lazily uncreative) and produce a rendition of the original!! Can u imagine the original being on high rotation (played every now n then) plus the renditioned advert on probably every half an hour...dont know about any of u but I know that radio/Tv would lose my listenership.”
Cindy hakuishia hapo ambapo aliendelea kwa kusema, “Mental and emotional appeal goes way further than just a popular melody...it’s the msg thats left behind after the melody stops n another commercial comes in before a chain of other programming activities. Small research...go ask ten ppl who listened to the radio in the morning n ask them the msg they got from any of the copy music adverts... I did n I know what I gushin about!!!”
Miongoni mwa nyimbo za wasanii wa Bongo Flava zilizotumiwa kufanya matangazo ya simu ni pamoja na Hakunaga wa Sumalee, Nimpende Nani wa Diamond, Mgambo wa Juma Nature (Vodacom), Bongo Flava wa Dully Sykes (Tigo), Dushelele wa Ali Kiba na Ndege Mtini wa Ferooz (Airtel).

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates