Tom Cruise ndiye muigizaji anayelipwa hela nyingi duniani


Licha ya kuwa kwenye mchakato wa kupewa taraka na mke wake Kate Holmes, muigizaji wa Mission Impossible  Tom Cruise ametajwa kuwa muigizaji anayeingiza fedha nyingi zaidi duniani.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes, Cruise ameingiza kiasi cha dola milioni 75 kati ya May 2011 hadi May 2012.
Amewapiku waigizaji wenzie Leonardo DiCaprio na Adam Sandler ambao wamekamata nafasi ya pili katika orodha ya waigizaji 100 wanaolipwa pesa nyingi zaidi.

Adam Sandler
Leonardo DiCaprio  
Cruise mwenye miaka 50 amefanikiwa kuingiza fedha nyingi kwa kufanya vizuri kwa filamu yake ya  “Mission Impossible – Ghost Protocol” iliyotengeneza dola milioni 700 kwenye majumba ya sinema.


DiCaprio na Sandler wamekamata nafasi ya pili kwa kuingiza dola milioni 37 kila mmoja.

Mcheza mieleka wa zamani Dwayne ‘The Rock’ Johnson amekamata nafasi ya nne kwa kuingiza dola milioni 36 baada ya miongoni mwa filamu alizoigiza Fast Five kuingiza dola milioni 626 za box office.

The Rock


Ben Stiller
Sacha Baron Cohen 
Mchekeshaji Ben Stiller amekamata nafasi ya tano kwa kuingiza dola milioni 33 huku Sacha Baron Cohen akifuatia kwa kuingiza dola milioni 30.
Wengine waliopo kwenye top ten ni Johnny Depp, 7, Will Smith, 8, Mark Wahlberg, na Taylor Lautner, 10.




Jonny Deep

Will Smith
Mark Wahlberg
Taylor Lautner

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates