Pepsi yawamezea mate Camp Mulla




Kampuni ya SBC Kenya Limited imedaiwa kuwamezea mate Camp Mulla ili wame sura za kinywaji cha Pepsi.

Kama ikiwachukua itakuwa na uhakika wa kampeni yake kuwafikia vijana wengi wa Kenya ambao wanalizimia kundi hilo.

Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Star kuwa Pepsi wanalitaka soko la vijana na  Camp Mulla wako juu sana sasa hivi hivyo hiyo itakuwa ni rahisi kwa kinywaji hicho kuongeza umaarufu kupitia wao.

Camp Mulla linaundwa na vijana watano, Taio Tripper - Matthew Wakhungu, Shappa Man - Benoit Kanema, Miss Karun - Karungari Mungai, K'Cous - Marcus Kibukosya na mwanzilishi Mykie Tuchi - Michael Mutooni.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates