Msanii wa bongo flevah
nchini Tanzania maarufu kama Timbulo amesema anategemea kutoa wimbo wake
mpya siku chache zijazo ambao amewashirikisha kundi la X-maleya kutoka
nchini Cameroon.
Miezi kadhaa iliyopita
Timbulo aliandamwa na maswali mengi yaliyoambatana na maneno ya
kumshutumu kuwa ali copy na kupaste nyimbo zake mbili zilizopita "Domo
Langu" na "Waleo Wakesho" kutoka katika nyimbo za kundi hilo.
Kwa mujibu wa maelezo ya
Timbulo alidai kuwa haku copy bila idhini ya wenye nyimbo kama
inavyodhaniwa na wengi, bali alipewa ruhusa na X-Maleya wenyewe na
vithibitisho vyote anavyo.
Timbulo ameendelea
kusema kutokana na kwamba anawa feel sana X-maleya na wao wanam feel,
sasa ameamua kuwashirikisha kabisa katika wimbo wake mpya aliouita "Lastic ya Upendo"
inayotegemewa kutoka hivi karibuni na tayari wameshamtumia demo yenye
sauti zao na ya Timbulo na kinachosubiriwa sasa ni mixing imalizike.
Kupitia ukurasa wake wa facebook Timbulo leo ameandika: " Habar njema ni kwamba wimbo mpya tayar upo
mkonon, waitwa Lastic ya upendo nimefanya na x-maleya, a group music from
cameroun, ambao nimewah kutajwa kuiba nyimbo kutoka kwao,,,!".
Leotainment
ilimuuliza Timbulo juu ya mpango wa video ya wimbo huu aliyowashirikisha
wasanii kutoka nje ya Tanzania, na hiki ndicho alichojibu:
" Wao X-maleya
walitupa option tatu za kufanya video, option ya kwanza ni wao watutumie
clips za parts zao walizoimba katika wimbo huu watakazo shot huko kwao.
Option ya pili ni sisi tusafiri kwenda Cameroon kushot huko, na option
ya tatu ni wao waje Tanzania tushot hapa. Sasa mpango mzima utafahamika
mara baada ya audio ya wimbo huu kuwa released wiki ijayo kama mixing na
mastering itakuwa imekamilika, lakini uamuzi wa kufanya video utatoka
katika hizo option tatu".
Kazi hii ya "Lastic ya upendo"
imetengenezwa katika studio ya Combination Sound chini ya producer Man
water, lakini mixing inafanyika hapa Tanzania na Cameroon kisha
watachagua ile itakayokuwa nzuri zaidi kwa ajili ya official release.
Home »Unlabelled » Baada ya kushutumiwa ku-copy nyimbo, Timbulo sasa apiga collabo na X-maleya wa Cameroon.
Baada ya kushutumiwa ku-copy nyimbo, Timbulo sasa apiga collabo na X-maleya wa Cameroon.
By Unknown • 12:02 PM • • Comments : 0
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment