Chris Brown amuajiri Karrueche Tran kuwa designer wake wa nywele na nguo


Inaonekana kama hit make wa don’t wake me up Chris Brown hajakubali kabisa kuwa mbali na ex girlfriend wake Karrueche hata kama sio kimapenzi tena.
Kwa mujibu wa Hip Hollywood Chris alimpa ajira kuwa stylist wake, na Karruache Tran aliipokea ajira hiyo na kumdizainia mtindo wa nywele kwa ajili ya kufanya photo shoot inayoonekana ni the latest kwa Chris. Ajira hii inasemekana kuwa haina mahusiano na maisha yao ya kimapenzi bali ni kama wameamua kufanya biashara tu kwa kuwa Chris anahitaji designer na K.T ni mkali upande huo.
Watu wa karibu wa wawili hao wameendelea kukanusha kwa msisitizo kuwa hakuna kinachoendelea kati yao na kwamba Chris Breezy bado yuko na Rihanna wake na anavyokuwa karibu na K.T haimaanishi kuwa wanataka kurudisha mahusiano yao.
Kwa kawaida inaleta maswali kwa wengi hasa ukizingatia Chris alitamka hadharani tena kupitia video aliyoirekodi kuwa anampenda pia Karrueche japo inabidi tu amuache ili aende kwa Rihanna, na hivi karibuni walionekana anatoka kwake akiwa na K.T na kumsindikiza na ikasemekana mrembo huyo alienda kuchukua vitu vyake kwa Chris asepe kwa amani. Ila hii sasa ya kumpa ajira ya kuwa stylist wake katisha zaidi.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates