Akon amsaini Konvict mtoto wa mtaani kutoka kenya mwenye miaka 14, story yao ni kama movie.


Wiki hii imeanza na zali zaidi ya lile la mentali kwa mtoto ambae alikuwa anaishi katika mazingira magumu sana nchini Kenya, inaweza kuwa ndoto alizoota zikmekuwa kweli na kama hakuwahi kuota basi Mungu amemsapraiz na kujikuta anapata deal la uhakika la kufanya muziki chini ya lebel kubwa duniani ya ‘Konvict’.
Mtoto huyo anaeitwa Wilson alimsimamisha Akon wakati anaelekea kupiga show pande hizo na akaona kabisa kuwa hii ilikuwa ni chance ya yeye kumueleza Akon ya moyoni tena sio kumuomba mkwanja ila ni kumuomba kujiunga na lebel ya Konvict. Duh, unaweza kudhani mtoto huyo alikuwa mwehu eeeh…dogo alirusha mkuki vizuri!!
Baada ya Akon kukubali kusimama tu mtoto huyo alizitumia dakika chache kumsimulia hali mbaya ya maisha anayoishi na jinsi ambavyo baba yake alivyomtesa na kulazimika kulala nje, akaeleza jinsi gani anavyoupenda muziki na hana jinsi ya kuweza kuingia studio kurekodi. Surprisingly, Akon akaamua kumpa nafasi, akaingia nae kwenye gari lake na wakaelekea wote kwenye concert yake.
Hatujui nini kiliendelea kwenye gari lakini inaonekana waliendelea kuongea kuhusu yale waliyoyaanzisha. Na haikuwa raisi kwa Akon kumpa nafasi kirahisirahisi tu.
Wakati anaendelea na performance yake mkali huyo toka Senegal alimuita stejini yule mtoto. Kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa kubwa na Akon, dah, hii ni bahati ama baraka?! Akon akamkabidhi dogo mic na kumwambia aperform!
Ni kama ulikuwa mtihani wa mwisho kwa dogo huyo ambao ungemtoa lawama Akon kirahisi, dogo alifunika vibaya na kuonesha kipaji kikubwa alichonacho.
Haikuhitaji press release ama press conference kutangaza uamuzi wa Akon, alishika mic na kutangaza mbele ya umati wa watu, “Wilson the newest member of the Konvict family”. Ni hivyo tu dogo anachukua pipa kwenda kuishi ndoto zake Marekani.
Huyu ni mtoto wa kiafrika mwenye story ya mafanikio inayofanana na ya Akon.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates