Hereni za kumsapoti Obama alizovaa Beyonce zampa deal mtengenezaji, aongeza mauzo ya hereni kwa kasi, apata order dunia nzima.


Ni usanii na ubunifu uliofanywa na designer mmoja wa mambo jewelries aliyetengeneza hereni ambazo wanawake walitakiwa kuzivaa ili kuonesha kuwa wanamsapoti Barack Obama katika uchaguzi wa uraisi wa Marekani, ambae aliuza kidogo sana mwanzoni lakini mambo yamebadilika mara tu baada ya Diva Beyonce kuzivaa hereni hizo.

Beyonce akiwa amevaa hereni hizo
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ designer huyo anaeitwa Erika Pena amesema tangu azitengeneze alikuwa ameuza pea 5 tu lakini tangu Beyonce azivae hereni hizo jumamosi iliyopita ameshauza pea 1,300 na anazidi kupata order kutoka sehemu mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na Uingereza, Uswizi, Chile, na Argentina, lakini order kubwa sana inatokea Uingereza.
Bei ya pea moja ya hereni hizo ni dola 32…ambazo ni karibia 50,000 za kibongo.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates