Rihanna na Karrueche wanaona poa kuchangia penzi la Chis Brown!


Mkasa wa mapenzi yenye pembe tatu zinazowahusisha warembo wawili Rihanna na Karrueche Tran kwa 'Don’t wake me up' hit maker Chris Brown unazidi kunoga siku hadi siku na imesemekana kuwa warembo hao wako poa tu na maisha yao na ‘baby boy’ wao Chris Breezy.
Mtu mmoja ameiambia Hollywood Life, “he got them both twisted up. He is trying to get as much p-y as he can before he leaves next month.”
Chanzo hicho kiliendelea kufunguka, “Chris anawapenda kweli wote na wanajua hilo na wao wanampenda pia”, akaendelea, “it’s crazy situation. Na inafanya kazi kwao, na ni kama RiRi na K.T wako poa tu na hili, hivo ndivyo ilivyo.”
Lakini stori za mtaa kwa upande mwingine zilisema Rihanna aliogopa pale alihisi kuwa labda Chris angeenda na Karrueche T kwenye party yake kubwa ya Halloween iliyowakutanisha mastaa kibao jumatano ya wiki hii.
Mtu mmoja alisema, “ingawa the 'umbrella' hit maker RiRi alikuwa poa tu kwa kile kinachoendelea kati ya Chris B na K.T lakini hakuwa na uhakika kama Chris ataamua kwenda kwenye party yake na K.T na hii ni kutokanana tetesi ambazo zilikuwa zimetapakaa mitaani na kwenye mitandao kuwa huenda Chris akatokea pale akiwa na K.T kama kawaida. Hapo ndo utaona kweli mapenzi ya watatu hayawezekani hasa inapoonekana kuwa itabidi kukutana kwenye eneo moja.
Chis Brezzy alitangaza kuachana na Karrueche October 4, na kauli yake ilikuwa ,” nimeamua kuwa single ili nifocus kwenye kazi yangu. Nampenda sana Karrueche lakini sitaki kumuona anaoumia kwa sababu ya urafiki wangu na Rihanna. Badala yake inabidi niwe single ili Kurusu kila mmoja wetu kuwa na furaha.”
Siku chache zilizofuata Chris B alitoa video ikiwa na kauli nyingine inayoonesha kweli anawapenda wote Rihanna na Karueche na hajui afanye nini na hajui kama kweli inawezekana kuwapenda watu wawili lakini ndivyo yeye anavyojisikia, lakini mwisho wa siku ikaonekana kabisa ameamua kuhamia rasmi kwa Rihanna wake wa zamani na kumtangaza rasmi japo ndo hivyo tena hawaachani na Karrueche pia. 

Haya ndiyo yanayoitwa Triangular Love, “mapenzi ya pembe tatu”.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates