Nas augua ghafla ashindwa kutokea kwenye show, alilazwa kwenye chumba cha dharura Hospitalini


Rapper mkongwe Nasir bin Olu Dara Jones a.k.a Nas alishindwa kuhudhuria jana kwenye show yake ambayo ilikuwa inarushwa live kwenye kituo kimoja cha television kinachorusha show maarufu "Live with Kelly and Michael!"

Nas kupitia account yake ya tweeter aliwa-update fans wake kuhusu hali yake ya afya kuwa ilimbidi akimbie kwenda hospitalini muda huo na kuwaomba radhi kwa kutoonekana kwenye show.

Tweet yake ya january 11 inasomeka hivi, "Peace y'all. I'm out of the ER & doin alright. I'm on bed rest for a few. Apologies to everyone @ Live w/ Kelly & Michael. I'll make it up.."
Japokuwa 'hate me now' hit maker hakusema alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa aina gani, baadhi ya blogs za Marekani ziliandika kuwa alikuwa anasumbuliwa na Flu, na kwa mujibu wa 'The YBF' watu wa karibu wa Nas walimwambia mtangazaji msaidizi wa television show ya "Live With Kelly & Michael" kuwa Nas alikuwa na Stomach flu.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates