Grandpa yamnasa Kenrazy

Lebo ya muziki inayokuwa kwa kasi sana Afrika Mashariki, Grandpa kutoka Kenya, imefanya hatua nyingine ya nguvu kwa kumsaini nyota mwingine mkali wa muziki wa nchi hiyo, Kenrazy ambaye sasa anaungana na timu hiyo ambayo siku hadi siku inajizolea heshima kwa kazi nzuri inazofanya.


Huu ni ujio mpya na wa faraja wa Kenrazy ambaye wengi walikuwa wakifahamu kuwa amekwishastaafu muziki, ambapo hatua ya msanii huyu kuingia Grandpa imeenda sambamba na kuachia kazi mpya inayokwenda kwa jina 'Vitambi'.

Kenrazy bado anajulikana kwa ngoma yake kali ambayo inakwenda kwa jina Ti-Chi, na sasa akiwa chini ya Grandpa, Msanii huyu anatarajiwa kurudisha heshima aliyokuwa nayo katika muziki katika ngazi aliyokuwa amefika hapo awali na zaidi.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates