MMILIKI WA SHAROBARO RECORDS ATEMWA NA MKE WAKE.

Mkali wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa ametambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Bashasha aliyempa shavu Vanesa amesema kuwa ameachana na Mkewe ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa Kiume.


  
Msanii Bob Junior akifunguka kupitia Kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio amesema kuwa ameachana na mkewe kwa sababu ya wivu wa Mapenzi aliyokuwa nao huyo ambaye alikuwa mkewe ambaye ameweza kumzawadia Bob Junior Mtoto Mmoja wa Kiume.

Bob Junior amefunguka na kusema kuwa wale wote waliosema kuwa alioa ili aweze kupikiwa kipindi cha mfungo si kweli bali wameshindwana na mkewe kwa sababu za Kifamilia na Wivu wa Mapenzi,lakini mkali huyo hajaishia hapo bali amekaribisha Maombi kwa yoyote ambaye atakuwa tayari bali anapaswa kuwa na Tabia njema

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates