SIRI YA MCHEZO LYRICS

SIRI YA MCHEZO LYRICS
Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/sikuwa na  umuhimu kihivyo… stimu  zikanipa elimu ya Biko/ Kimaandiko… kimistari.. hadi fans wanascream nikirap../  sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop/

Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa  #teamMabiiitoz  /
Achana na  power window.. sijui  rimz za dimpoz/
haileti bingo, mshiko?  Star ishi simple/   sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/
wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui  kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/ bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/
jikombe ugongwe…mtaaa  ukuone hauna ishu/
ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda/
Usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi.. je hizi track za  harakati ni ujinga?/
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji/  na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati..sio kipaji  kama  Kubanda eti unachana kigumu/  kisa  track ikivuma sana kwenye chati  haidumu /
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa SOKO HURIA../  baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA/NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI../  najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?/ labda kubisha na wakinitisha najihami../  inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani/
‘’Pole MAPROSOO’’ ( uhujumu –uchumi ) umefanya umetubu.. / WAZEE ni  wahuni  hadi soo waay back before SUGU/
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu/ na MBWA MWITU wenye siri.. ili bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../  huo ni utumwa pia/Unafanya  vijana  wanaumia../
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia..

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates