DROGBA, EBOUE MATATANI KWA KUOMBILEZA KIFO CHA MANDELA DIMBANI


KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Uturuki-TFF linatarajia kuwahoji nyota wawili wa kimataifa wa Ivory Coast wanaocheza klabu ya Galatasaray, Didier Drogba ba Emmanuel Eboue kufuatia kuonyesha ishara katika mechi ya kumkumbuka rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliyefariki dunia Alhamisi. 

Baada ya Galatasaray kushinda mabao 2-0 dhidi ya SB Elagizspor katika mchezo wa Kombe la Ligi Ijumaa, nyota hao wawili walivua fulana zao na kubakia na vesti zilizokuwa na ujumbe kuhusu Mandela. Mara baada ya Drogba kuvua fulana yake vesti aliyokuwa amevaa ndani ilikuwa na maandishi yaliyosema “Thank you Madiba” akimaanisha asante Madiba wakati vesti ya Eboue ilikuwa na maandishi yaliyosomeka “Rest in Peace Nelson Mandela” akimaanisha pumzika kwa amani Nelson Mandela. TFF linakataza kuonyesha fulana yoyote yenye ujumbe unaohusiana na mambo ya siasa wakari wa mechi ya soka.

Mmh - nionavyo mimi hii sio siasa kwa kua Dunia nzima imeomboleza kwa namna zao juu ya kifo cha Madiba, kama wataadhibiwa nadhani itakua ni kuwaonea. Inawezekana Mandela asiwe na maana yoyote kwa chama cha mpira wa miguu cha Uturuki lakini kwa Drogba, Eboue na Waafrika kwa ujumla Madiba ni muhimu sana.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates