IJUE ORODHA YA WASANII 20 TANZANIA WENYE UKARIBU MKUBWA SANA NA MEDIA KWA KUTHAMINI NA KUJALI INTERVIEWS

MWAKA  2013, Tunaumaliza  katika kiwanda hiki cha burudani  yapo mengi ambayo nisipoyasema nitakuwa kama naendelea kuweka sumu katika moyo wangu na pia kushindwa kuwasaidia wale ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakiamni kuwa mafanikio ni dharau nakushindwa kutoa ushirikiano wa dhati pale unapohitajika  kutokana na kazi wanazofanya .

kwa moyo wa dhati kabisa  nina kila sababu ya kuwashukuru  na kuwaelezea  WASANII WAFUATAO AMBAO WAMEKUWA NI MFANO WA KUIGWA TANZANIA  KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE  NA MUNGU AZIDI KUWABARIKI KATIKA KILA WANACHOKIFANYA .

NI KATI YA WASANII AMBAO NAWEZA KUWAWEKA KATIKA KUNDI LA WACHACHE WENYE KUJUA UMUHIMU WA MASHABIKI, UMUHIMU WA WADAU  NA PIA UMUHIMU WA RADIO  ZA MIKOANI.
          
        
                                    1:DARASA:
 Jamaa kwa upande wa kazi amekuwa akifanya vizuri sana , kiasi cha kuwa tishio kwa wale ambao walikuwa wanaaminikia katika upande wa hip hop  hapa nchini . sijui ni nidhamu ya kazi au vipi lakini mafanikio yake yanaonekana kwa namna moja ama nyingine  tangua ameanza kufahamika  na ngoma yake ya SIKATI TAMAA hadi hii leo katika ngoma ya WEKA NGOMA aliyofanya na Ditto . Darasa ni msanii ambaye anajua umuhimu wa media , na nidhamu ya kazi anayo. ni msanii ambaye yupo tayari kwa  interview wakati wowote, muda wowote ,  mahali popote  na anatoa ushirikiano wa kutosha , nakiri, sijawahi  msikia mtangazaji yoyote akicomplain  juu ya huyu jamaa ,et ametafutwa katika interview akajibu mbovu, akaacha kupokea simu au vipi  , hapana  aseee, na ni kati ya wasanii wanaofunguka katika interviews hadi mtangazaji unapata  hamu ya kuendelea  kumuhoji     
                                     
                                           2: P THE MC (tamaduni muziki)
msanii mwingine huyu,  ambaye  muda wowote yupo tayari kuzungumza chochote ambacho utahisi unataka ufafanuzi kutoka kwake , au kujua lolote juu ya kazi zake, naweza sema ni aina ya msanii ambaye yupo tayari kwa wakti wowote  kuongea na media.

                              3:Zaiid  Mnete (tamaduni muziki)
sijui nisemeje juu ya huyu jamaa lakini waliofanya nae interview zaidi mnete wanaweza kumzungumzia vizuri zaidi , maana ni aina ya msanii  ambaye katika swala zima la utayari  yupo tayari, na nafunguka zaidi ya maelezo , ni mfano wa p the mc, darasa na wengine asee, hata umpigie simu yupo kwenye gari au kalala Zaidi mnete lazima atapokea.  hongera sana .
                                           

                           4: Azma  Mponda (tamaduni muziki)
naye siwezi acha kumzungumzia  jamaa, amekuwa na nidhamu sana ya kazi , nidhamu za media na kujali vile vile. mpigie muda wowote, popote akishajua lengo na makusudi ya simu yako atakupa ushirikiano  wa kutosha .           

                                             

                                  5:LAWIZE  INTERTAINER :
Huyu ni kati ya wasanii ambao sitaacha kuwazungumzia  kabisaa, ni msanii ambaye anapigana kuhakikisha anafahamika  na kazi zake zinafahamika , msanii ambaye anajali , anajituma ,ana nidhamu ya kazi na anajali  na kuheshimu radio ndogo na kubwa . Lawize  ni msanii ambaye sijui nitumie lugha gani lakini wengi ni mashahidi juu ya hili, hakuna mtangazaji hata mmoja wa radio ambaye hajawahi kumzingumzia vizuri  lawize labda awe  hamjui .
                                                        
     

                                       6: NEY WA MITEGO:
Salute kubwa kwake , mpigie muda wowote, wakati wowote hata kama ana drive Ney atapokea simu ataweka pembeni gari mtapiga interview, kiukweli kutoka moyoni anajali vibaya mno jamaa, na ndo maana anazidi kujiongezea  mashabiki wengi .
                                                         

                                 7:NEIBA
duh! huyu naye ni kati ya wasanii hao hapo juu, hakuna siku utampigia simu utake interview Neiba akwambie hana nafasi au  hana muda , anajitoa zaidi ya maelezo , majivuno , majidai ya kutokuhojiwa , asee jamaa  hana kabisaaaaaaaaaaaa amini hilo.
                                                        

                                          8: DYNA NYANGE
yes, anajua umuhimu wa kuzungumza na mashabiki wake , kiufupi anajali na kuthamini interview , ukimtafuta hupati usumbufu kabisaaaa wa kumuhoji, tofauti na wengine, mara siwezi, mara tutafanya wakti mwngine, mara sina mudi, , lakini Dyna  hayupo hivyo.
                                                      

                                      9: RIYAMA
NI msanii ambaye ananivutia sana binafsi katika filamu za kibongo acha niseme ukweli, ni msanii ambaye ana nidhamu ya hali ya juu  , anajali,  na thamini, na ana adamu yiliyopitiliza. pigie simu popote , kokote , weka nae ahadi ya kufanya interview, suhirikiano atakaokupa , mwenyewe utashangaa. kiukweli yupo vizuri sana tofauti na wengine .
                                                           

                                    10:ABRA MBILIMBILI:
huyu anaingia tena katika list yangu ya wasanii ambao ni wepesi wa kufanyiwa interview katika media  na wepesi wa kutoa ushirikiano wa kutosha . jamaa kwa chochote ambacho utamuuliza ,iwe scandal iliyosukwa au  ya kawaida , atakupa ushirikiano wa hali ya juu.
                                                    

                               11:  STOPPER  RYMECCA:

na yeye stoper siwezi muelezea zaidi lakini jua ni kati ya wasanii wenye sifa ambazo nimezitaja kwa wengine wote hapo juu . huwa anatoa ushirikiano sana  katika interview , muda wowote na kwa chochote. big up sana kaka  ,nakukubali  mpaka pumzi ya mwisho.
                                                     

                            12: NIKKI WA PILI
siwezi muelezea zaidi lakini jua ni kati ya wasanii wenye sifa ambazo nimezitaja kwa wengine wote hapo juu . huwa anatoa ushirikiano sana  katika interview , muda wowote na kwa chochote. big up sana kaka  ,nakukubali  mpaka pumzi ya mwisho
                                                   

                         13:ROMA MKATOLIKI
hakuna ambacho utamuuliza Roma aache kukupa  ushirikiano kwakweli, katika interviews ambazo nimepiga naye  juu ya kazi na harakati zake ushirikiano kwangu toka kwake ulikuw amkubwa sana  , siwezi muelezea zaidi lakini jua ni kati ya wasanii wenye sifa ambazo nimezitaja kwa wengine wote hapo juu . huwa anatoa ushirikiano sana  katika interview , muda wowote na kwa chochote. big up sana kaka  ,nakukubali  mpaka pumzi ya mwisho.
                                                        

                          14: K  WA MAPACHA
hili ni jembe lingine tena , yaani ni zaidi ya sana , K wa mapacha   ndo aina ya wasanii wote waliopo hapo juu
                                                     

                        15:MRISHO MPOTO
kama unavyomuona ndivyo alivyo, si mtu wa maringo , si mtu wa majidai , popote yeye atakupa ushirikiano tu wa hali ya juu ya
                                          

                           16:JOH MAKINI
 kifupi  hana dharau , we jua hilo tu

                                                                

                          17:LINEX
linex nikianza kumzungumzia siwezi maliza leo,  lakini waliopo katika media na waliowahi kufanya naye interview wanaweza wakanisaidia kusema juu yake , ni aina ya msanii ambaye  hana mizinguo katika interview , maringo o s majibu ya ajabu ajabu kama wengine , tena huyu wakati mwingine anatafuta watangazaji kwaajili ya kutaka kuongea na mashabiki wake waliommisi labda kwa kipindi Fulani.

                                                                 

                        18:JCB
ni real nigger , ni real  hip hop , namkubali  hadi mwisho. Amekuwa  wepesi kufunguka sana juu ya interviews mbalimbali katika radio , iwe mchana au usiku, nakumbuka wakati anasafiri kwenda ufaransa , jamaa yupo airpot kabla ya kuondoka  nilimuomba sana dakika hata mbili tu ya kuzungumza nae juu ya safari yake, lakini  hakusita wala kuzingua na badala yake laifunguka hadi mwisho, kitu amvachjo mwingine au wengine wasingeweza au wasingekubali. KAKA NAKUHESHIMU SANA .
                                                         

                       19:GNAKO
Dah! Nakosa mameno kabisa ya kuzungumza  juu ya Gnako , ila ni zaidi  ya kujali  na kuthamini, jamaa akishagundua ni simu ya interview  au uwe umempa taarifa juu ya interview kwakweli we tegemea mengi kutoka kwa jamaa.
                                             

                     20:KALA JEREMIAH .
kichwa kingine katika interview, kala jeremiah anafanikiwa kwasababu ya nidhamu katika kazi ,kujali mashabiki,  kujali media ndogo na kuzipa  ushirikiano .  ni mwepesi sana wa interview  na ana utayari kwa hilo kwa muda wowote .

 ORODHA HII YA WASANII 20  WALIOPO HAPA , NI  KWAMUJIBU WA INTERVIEWS AMBAZO WAMEKUWA WAKIZIFANYA , NA NAMNA AMBAVYO WAMEKUWA WAKIJALI NA KUTHAMINI NA KUTOA USHIRIKIANO WA KUTOSHA , NI WASANII WANAOJALI  NA KUONA UMUHIMU WA  MEDIA KWAO  NA KATIKA KAZI WANAZOFANYA ZA KIBURUDANI, MATAMASHA NA MENGINEYO.

HICHO NDICHO KINACHOWATOFAUTISHA WASANII HAO HAPO JUU NA WENGINE  AMBAO HAWAPO KATIKA ORODHA HII.
WASAA  WALIOACHWA HAIMAANISHI HAWANA UTAYARI WA KUFANYA INTERVIEWS KATIKA  MEDIA AU KUONGEA NA MASHABIKI WAO HAPANA , ILA YAWEZA KUWA UPATIKANAJI WAO  UMEKUWA NI WASHIDA SANA  UKIAMBATANA NA  MAJIDAI MENGI  PAMOJA NA KUTOJALI.

KUNA BAADHI YA WASANII WANAPOPIGIWA SIMU  WAKATI MWINGINE   HAWAPOKEI , NA HII SI MARA MOJA  UNAWEZA KUTA NDO TABIA YAKE, WAKATI MWINGINE  WENGINE WANAKUWA NA UTAYARI WA INTERVIEW LAKINI WANAPOTAFUTWA  SIMU HAZIPOKELEWI AU WANAKUWA HAWAKO  TAYARI KUZUNGUMZA CHOCHIOTE.

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates