KWA NINI NAWAPENDA WANAWAKE....

.
Mme na mke walikuwa wamekaa wanatazama TV
mara mke akasema, “Ushakuwa usiku sasa,
nimechoka ngoja nikalale”
Akanyanyuka na kwenda jikoni akawaandaa samaki
wa chakula cha siku ya pili mchana, akapika chapatti
kwa ajili ya chai ya siku ya pili asubuhi kisha
akachemsha chai kwa ajili ya watoto asubuhi.
Akaiandaa meza na kuweka kila kitu muhimu kama
vile vijiko, vikombe, sahani, cocoa, majani ya chai nk
kwa ajili ya chai ya asubuhi.
Kisha akaingia ndani na kuandaa nguo za kuvaa
mmewe asubuhi na watoto wake waendao shuleni,
akaja sebuleni na kuondoa makaratasi na kuweka
vitu sawa baada ya watoto kuvichezea, Akachukua
simu na kuzichaji akaweka kila kitu sehemu yake.
Akajinyoosha ili aende kitandani lakini aka kaka mezani
na kuandika karatasi ya kumkumbusha kwenda
shuleni, akachukua kadi na kuandika kwa ajili ya
kuwatakia birthday marafiki zake siku ya pili na
kuziweka kwenye bahasha.
Akaorodhesha mahitaji ya kuchukua sokoni siku ya
pili yake akitoka kazini na kuweka vitu vyote karibu
na mkoba wake. Akaingia bafuni akauosha uso wake
na kujikausha, akapiga mswaki ….. Mme akamwita,
“Nilifikiri umeenda kulala kumbe bado.” “Ndio nataka
kulala sasa,” akajibu.
Akanyanyuka na kwenda kuhakikisha milango yote
imefungwa na kuifunga. Akapita chumba cha watoto
na kuweka neti vizuri na kuongea na mmoja
aliyekuwa akimalizia kazi za shule.
Akawategea kengele ya saa ya kuwaamsha asubuhi
wasichelewe kujianda na kuhakikisha taa zimezimwa
na radio pia akarudi chumbani kwake na kuweka nguo
zake vyema za kuvaa kesho yake. Kisha akasali na
kumshukuru Mungu kwa kumaliza majukumu ya siku
salama.
Mme yeye alisimama pale alipokuwa amekaa
akitazama TV, akaizima TV na kujisemesha, “Naenda
kulala sasa" bila kujua anamwambia nani muda ule.”
Na akaenda kulala bila kufanya chochote wala kuwa
na wazo la kufanya chochote
Umeona umuhimu wa mwanamke hapa? ujumbe
huu kwa kuonyesha umuhimu wa wanawake …
Wao ni chimbuko la furaha zetu na mafanikio yetu…
ujumbe huu usomwe kwa kila mwanamme ili nao
waone umuhimu wa mwanamke katika Maisha
yao……!!!
Amen

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates