MKURUGENZI WA BOMBA FM RADIO ZANZIBAR AMEAMUA KUTANUA WIGO WA MZIKI WA ZANZIBAR.SOMA HIIGuru Ramadhani. Mkurugenzi Bomba fm Zanzibar.


Mkurugenzi mtendaji wa Radio bora hapa zanzibar  Bomba fm Radio GURU RAMADHAN aliwaambia wafanya kazi wake katika kikao kilichofanyika mapema mwezi huu wa pili.Pamoja na Agenda nyingine ambazo nyeti zilizojadiliwa pia mkuregenzi huyo alidhamiria kuibua  na kuendeleza vipaji vya wanamuziki wa Zanzibar ambao kwa namna moja ama nyengine vipaji hivyo vinaonekana kupotea bure .Mkurugenza aliwataka waendesha vipindi vya burudani kulipatia mkazo hilo na kulitekeleza kwa umakini mkubwa.
Pia mkurugenzi amefanya mabadiliko ya vipindi kadhaa pamoja maboresho yake, sikiliza BOMBA FM RADIO zanzibar  ili ujue kilichobadilika mwaka 2014.
Maoni ya Watangazaji/Angalizo kwa wanamziki wa Zanzibar.

Uptowntz ilikutana na mtangazaji wa Breakfast Bomba MB The Swaga/Mb Doctor yeye alikua na haya ya kusema.


MB DOCTOR & PASHA.

MB. Doctor. Wanamuziki wa Zanzibar wanatakiwa kuboresha nidham zao ili kufikia mafanikio, pia aliwataka kuacha dharau kwa maana hakuna career ambayo inaweza kusonga mbele bila nidham ndani yake. Pia aliwataka wasanii kufanya kazi zenye ubora na kiwango cha juu ili kua na ushindani zaid katika soko la mziki Tanzania.

JABIR.Super Jay International.Host wa show za kiburu FRIDAY & SAT,DAY NIGHT GROOVE.Alitirirka ifuatavyo.


JABIR SUPER JAY

Mafanikio hayapatikani mara moja kama baadhi ya wasanii wanavyodhani hapa Zanzibar. Inatakiwa kila msanii anaejijua kua anakipaji ambacho kinahitaji kuendelezwa kama Radio hii ilivyodhamiria kufanya hvyo bac kuchukua jitihada binafsi kulinda na kutunza kipaji chake ili kupata mafanikio siku za usoni. Super Jay pia alisisitiza Nidham kwa wasanii. Pamoja na hayo yote alisema kuhusu fursa hii ambayo wasanii wa Zanzibar wanatakiwa kuitumia bila kuipoteza kwani huu ni moyo wa uzalendo ambao umeoneshwa na mkurugenzi wa Bomba fm Zanzibar.
Pia muandishi wa Blog hii alikutana na msanii wa mziki wa kizazi kipya toka maeneo ya fuoni Dogo fani alipoomuuliza kuhusiana nidham mbovu za wasanii yeye pamoja na wenzake dogo fani ilikiri kua kweli kuna baadhi ya wasanii wanadharau na akasema kua wasipobadilika na kujitunza watashindwa kuzitumia fursa kama hizi ambazo zinatolewa na Bomba fm. Ameenda mbali zaidi na kumpongeza mkurugenzi wa Bomba fm katika jitihada zake za kuboresha mziki huu.

KAZI KWENU WASANII KUFANYA KAZI NZURI NA BORA ILI FURSA HII ISIPOTEE BURE.

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates