LOVE STORY - JIFUNZE KULINDA AHADI YAKO KWA UMPENDAE

Miaka kumi na mbili iliyopita binti huyupichani aitwaye Dear alikuwa namahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja wakiwa na umri wa miaka 18.Walipendana sana na kuapiana kuwa

wasingesalitiana na kuja kuishi kwa pamoja kama mme na mke baada yakuhitimu masomo yao. Binti akatoa wazo kwa kuwa yeye hanaimani na wanaume, kwani wengi huwana tabia za kusaliti mahusiano basiwaape kwa kitumia Biblia na kofuli. Wazo hili kijana alilipokea kwa furahana binti akafurahi sana kuona yule kijana amekubaliana nae kuwa ataapakwa njia hiyo kama ishara ya kuwa hawatasalitiana na kupendana kwa
dhati. Wakaondoka wakiwa na biblia na kofuli
yao mpaka kwa mzee mmoja aliyeaminika kwa busara na kumweleza adhma yao naye kabla ya kuwakubalia ombi la kuwa shahidi wao akawauliza, " Je ni kweli mmeamua kuapa kwa
kutumia Biblia na kofuli hii kuwa mnaufunga uhusiano wenu kuwa wenu tuu na mnakubali kuwa hamtasalitiana milele?" Wote wakajibu ndio. "Je mnatambua kuifunga kofuli hii na
ufunguo kuniachia mimi na kofuli kwenda kuitupa mbali mjue kamwe
hamtaifungua tena na matatakiwa kuwa pamoja kwa namna yoyote ile?" Wakasema tumeafikiana. Mzee akawaongoza kwa sala na kuwaomba waishi kama walivyokubaliana na kisha kuifunga ile
kofuli. Wale vijana wakarudi majumbani kwao
na kuendelea kuishi kwa furaha na amani huku kila mtu akiwa na kiu ya kuonyesha zaidi upendo kwa
mwenzake. Miaka ikaenda wakahitimu chuo na kijana akapangiwa kazi kijijini sana na
kukawa na matatizo ya usafiri na binti kwa kuwa alipangiwa mjini akawa kila mara akimtembelea kijana na kijana
akienda mjini pia. Miaka ikaenda hatimaye taratibu wakaanza kupunguza mawasiliano baada ya kijana kuhamishiwa mbali aidi na binti akabadili namba na kuanza mahusiano na boss wa kampuni
yake na kisha wakaoana. Kijana akafanya kazi kule kijijini kwa kujituma na kuweka fedha ili aweze
kuja mnunulia pete nzuri ya uchumba na harusi yao ije kufana na waishi vizuri bila kujua kuwa keshaolewa. Baada ya kujiandaa vya kutosha akaanza kuomba uhamisho ahamie mjini na alipofika mjini akapata habari
za mkewe kuolewa na wamehama mji ule.
Kijana aliumia sana na kisha akaamua kuondoka kwenda mbali kuanza maisha mapya akiwa na huzuni sana. Maisha ya furaha yakamwishia yule binti kwani hakupata mimba wala dalili na kila alipofanyiwa uchunguzi
akaonekana yupo safi. Furaha na amani ikaanza kumpotea katika familia yake na baadae mambo kuwa mabaya zaidi kabla ya kuanza kutembelea kila kibanda kilichoandikwa mganga wa jadi akihisi
kafanyiwa mchezo. Baada ya kwenda kwa njia hizo zote
bila mafanikio akawa hana jinsi zaidi ya kuwa mtu wa kulia na kuhuzukika kila mara. Siku moja akiwa ndotoni akaonyeshwa Biblia na ile kofuli akakumbuka kuhusu nadhiri yake na yule kijana. Akaanza
kumtafuta yule kijana amwombe msamaha na baadae akampata. Baada ya kumwambia kijana huku
akimwomba msamaaa kijana akasema mimi sina tatizo ndio maana sikuoa ili nikuone na uje uniruhusu kwa
kulingana na agano letu. Na kilichobaki hapa ni kumtafuta mzee kwani kofuli mimi nilimkabidhi mama
yangu na analo kwani niliamini mama ambaye ni mwanamke kama wewe angenirekebisha kama nikikosea na
ajue siri yangu na wewe ili azidi kunipa hekima na busara ya kuwa na wewe, je na wewe funguo ya akiba uliweka
wapi? Binti akasema niliipoteza nilipoanza mahusiano na mme wangu. Wakaenda kwa mzee na kusikia kuwa alishafariki, kijana akampa kofuli bila ufunguo na kumwomba binti ampe Ruhusa akaoe. Binti akakubali na kijana akaoa na sasa ana mke na watoto wawili lakini yule binti mpaka sasa kashaachika zaidi ya
ndoa nne akikosa amani kwa kuvunja
agano lake na kijana yule. Dada na kaka zangu kumbukeni 1. Kamwe usimwahidi mtu kumpa
mambo makubwa maishani na hali wewe huna uwezo 2. Kamwe usimwambie mwanamke
unampenda wakati humaanishi 3. Usitumie vitabu vya dini kufanikisha mipango yako ya ulaghai wa mapenzi 4. Kamwe usiwahusishe watu kukusaidia kushuhudia uongo ili kumpata mwanamke...Hawa ni viumbe ambao kwa asilimia kubwa sisi wanaume ndio huwafanya waumie na kila mwanamke katili,jambazi, kahaba na wengine lazima wana hadithi iliyowafanya kuwa hivyo na ilisababishwa na mwanaume 5. Usijaribu kufanya ahadi yoyote ili
kumpata mwanamke ukiapa kwa jina la Mungu kama huamini Ukishindwa kutekeleza huishia kukosa
furaha maishani mwako na kuwa kama dada yetu.


#chiwileinc entertainment

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates