TETESI ZA SOKA ZANZIBAR LEO JULY 28, 2016

Adeyum Saleh afagiliwa usajili wake wa kwenda Stand United, Wakala wa Mchezaji mpya wa Stand United Saleh Machupa ambae pia ni baba mzazi wa mchezaji huyo amesema mtoto wake amekwenda timu sahihi na yeye ndio aliemshauri kwenda timu hiyo baada ya kuondoka Coast Union ya Tanga ilioteremka daraja.

Mlinda mlango wa zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Suleiman Hamad ambae kwasasa anacheza timu ya Kijichi anatarajiwa kuondoka klabuni hapo na kujiunga na moja ya timu ya Ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwemo Mtibwa Sugar , wakati huo huo pia huwenda akarejea timu yake ya Zamani ya Black Sailors.

Timu ya Small Renger inayoshiriki ligi daraja la pili Wilaya ya Mjini ipo mbioni kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani Hafidh Ali “Mess wa Makadara” kwa gharama yoyote kutokea klabu yake ya sasa ya Muembe ladu.

Yahya Haji “karoa” mshambuliaji wa Villa United “Mpira Pesa” anawindwa na timu ya KVZ na JKU, mchezaji huyo amezisaidia kuzipa ubingwa wa Rolling Stone timu ya Mjini Zanzibar na Villa United Daraja la Pili Wilaya ya Mjini.

Mashabiki wa Soka Visiwani Zanzibar wameipa tano timu ya Kombain ya Mjini Zanzibar baada ya kuonesha soka safi katika mchezo wa kirafiki uliosukumwa jana usiku kwenye uwanja wa Amaan ambapo timu hiyo imepigwa 1-0 na Azam FC.

Mohd Ibrahim “Raza Lee” siku ya Jumamosi ya tarehe 30 July anatarajia kuinunua timu ya Taifa ya Jangombe kwa shs Milioni 35. Leo Usiku atafunguka LIVE kupitia kituo cha Radio cha Coconut FM 88.9 kwenye kipindi chao cha Coco Sports kuanzia saa 2:00 za usiku.

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates