MAISHA CLUB KUZINDUA USIKU MAALUM



 Maisha Club ya Dar es Salaam imeamua kuzindua usiku maalum ili kuweza kuwapa wateja vionjo mbali mbali.
Burudani hii itakayozinduliwa mwezi wa juni ni mwendelezo wa burudani ambayo hutolewa ndani ya ukumbi huu wa maraha.
Tarehe 7 Juni itazinduliwa usiku maalum wa FM Academia (Wazee wa Ngwasuma) ambapo atatafutwa mwanadada mwenye uwezo wa kulingwasimisha ndani ya maisha.
Alhamisi tarehe 8 juni itazinduliwa usiku wa Uzalendo plus na Twanga Pepeta ambapo kauli mbiu ni ‘tupende vya nyumbani’. Kutakuwa na burudani na vionjo mbali mbali kutoka makabila ya humu nchini. Uzinduzi utaanza na burudani toka katika kabila la Wahaya.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates