Lulu kama Diamond Platnumz, kuzindua Foolish Age mlimani City, soma hapa
Hatimaye mwanadada Elizabeth Michael (Lulu) yupo teyari kuachia filamu yake ya kwanza toka atoke jela, filamu aliyoipa jina la Foolish age inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 30 mwezi huu.
Akiandika kwenye ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii leo mchana lulu aliandika.
“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie ya mpya ya FOOLISH AGE....hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....
Filamu hii inasambazwa ka kampuni ya PROINPROMOTERS.
Huu utakuwa ni uzinduzi mkubwa wa filamu nchini baada ya msanii wa upande wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz kufanya shoo kubwa ya mziki kwenye ukumbi mkubwa na maarufu wa mlimani city jambo ambalo sio la kawaida kwa wasanii wa filamu na muziki hapa nchini.
Post a Comment