ay, July 16, 2012
Utoaji wa Tunzo, kwa Filam Zilizoshinda katika Tamasha la ZIFF la 15 katika viwanja vya Ngomekongwe.
MC Farouk akitowa utaratibu wa Usiku wa Utoaji wa Tunzo za
ZIFF, uliofanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe Usiku wa jana.
Wanafunzi wakisoma Utenzi wa Utoaji wa Tunzo kwa Filam Bora katika Tamasha la ZIFF la 15
Waziri wa Habaru Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbaruok, akitowa hutuba katika sherehe za Ufunganji wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar lilofanyika katika Viwanja vya Ngome Kongwe Forodhani na kuitangaza Zanzibar Kiutalii kupitia Tamasha hilo la 15 la ZIFF.
Mkurugenzi wa ZIFF akiwatambulisha wafanyakazi wa Tamasha hilo wote
wakiwa ni Wazanzibar waliofanikisha Maonesho ya Tamasha kwa sekta zote
katika kipindi chote cha maonesho hayo.
Wafanyakazi wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF, vijana wa
Kizanzibar wakiwasalimia Wananchi waliofika katika sherehe za ufungaji
wa Tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya ZUKU, akitowa salamu za Kampuni yake kuweza
kufanikisha Udhamini wa Tamasha hilo uliofanywa na Kampuni hiyo.
Mtayarishaji wa Filam ya UHLANGA kutoka Afrika ya Kusini Ndaaba
Ka Ngawane, akitowa shukrani kwa kupata ushindi wa Filam yake na kupata
ushindi wa jumla kupitia Filam hiyo
Mtayarishaji wa Filam ya LUHANGA kutoka Nchini Afrika ya Kusini akiwa
na Vijana wake baada ya kukabidhiwa Tunzo yake, na kuibuka mshindi wa
Jumla kwa kukusanya Tunzo nyingi katika Tamasha la mwaka huu la 15, kwa
ubora wa kazi yake kupitia Filam hiyo.
Mshindi wa Tunzo ya Filam ya Ruhago kutoka Nchini Rwanda Mbabazi Aime
Philbert akitowa shukrani kwa ushiindi wa filam yake baada ya
kukabidhiwa tunzo yake.
Waheshimiwa wakifuatilia vijana wakisoma Maulid ya Home wakati wa utoaji wa Tunzo za ZIFF.
Vijana wa Mtaa wa Mtendeni wakisoma Maulid ya Home katika Usiku wa Utoaji wa Tunzo za ZIFF kwa mwaka 2012
Watayarishaji na Wadhamini wa Tamasha la ZIFF wakipiga picha za
kumbukumbu ya Tamasha la 15 wakati wa Vijana wa Maulid ya Home wakisoma
katika Jukwaa la ZIFF la Ufungaji.
Mtayarishaji wa Filam ya ZAMORA kutoka Zanzibar Shamis Bhanji
akifurahiya Tunzo yake baada ya kukabiidhiwa kwa kuwa Filam bora kwa
Nchi za Afrika Mashariki.
Mwakilishi wa Kampuni ya ZANLINK akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa
Cheti cha kufadhili Tamasha hilo kwa Muda wa Miaka Kumi kutowa huduma ya
Internet kwa kipindi chote cha Tamasha.
Post a Comment