(Zanzibar, Julai 15, 2012).
Zuku usiku wa kuamkia juzi ilifanikiwa kuaanda warsha ya watengenezaji
filamu kutoka baadhi za nchi mbali mbali, ambao wanahudhuria Tamasha la
15 ya Zanzibar International Film Festival ZIFF.
Kauli
mbiu ya warsha hiyo ilikuwa “Kupandisha viwango vya ubora katika
filamu za kiafrika”. Wadau hao walilenga kuangalia kwa undani majukumu
mbalimbali kuanzia kwa wawekezaji, watangazaji, na wazalishaji kwa
lengo la kutoa ufumbuzi akinifu dhidi ya changamoto zinazoikabili sekta
ya wachezaji katika Afrika.
Warsha
iliyoendeshwa chini ya uenyekiti wa Firdoze Bulbulia, ilihudhuriwa na
wasemaji mashuhuri kama Ayuko Babu ambaye ni mtaalam wa filamu za
Afrika, Mahmoud Thabit Kombo, Mwenyekiti wa ZIFF, na Hannelie Bekker
kutoka Zuku.
Akitoa
maoni yake kuhusu kauli mbiu mbele ya jopo hiyo , Hannelie Bekker,
ambaye anasimamia vituo saba (7) vya; Zuku, alisema "Zuku itakuwa na
jukumu muhimu katika kupandisha viwango vya ubora wa filamu za kiafrika
kwa sababu inatoa nafasi kwa watengenezaji wa filamu na wazalishaji
kuuza na kuonyesha bidhaa zao. Aidha, Zuku hasa ina nia ya kukuuza
vipaji vya ndani na kutangaza kazi za wasanii wa ndani – na huo ndio
jukumu msingi wa uwekezaji wetu na uhusiano na ZIFF. Tunahitaji filamu
na tamthilia zenye bora na hii ina maana tuna maslahi ndio maana
tunataka kuona sekta hii ikistawi.”
Ayuko
Babu, ambaye pia alikuwepo kwenye jopo, alisisitiza haja ya
watengenezaji wa filamu kujipanga na kufanya kazi pamoja ili kuboresha
hali ya sekta ya filamu. Aidha alisisitiza haja ya kusaidia na
kuimarisha ZIFF. "Zanzibar ni mahali pazuri na kila mtu anaifahamu
hivyo kwa hiyo kuna umuhimu kwa kila mtu kujua kuhusu hilo na ZIFF ina
fursa ya kukua kama matamasha mengine ya kimataifa kama vile Cannes na
Ouagadougou." Pia alizitaka watengenezaji wa filamu kufikiri kwa makini
kuhusu mifano ya biashara yao ili kuhakikisha kwamba wanapata faida na
wanahakikisha kwamba wanawapa watu hadhithi zinazoleta manufaa.
Mwakilishi wa wacheza filamu, Farida Nyamachumbe alizungumza kuhusu changamoto alizokabiliana nazo ndani ya sekta.
Jambo
ambalo liliwavutia sana wasanii wa ndani ambao changamoto ya udhibiti,
uwekezaji na usambazaji ni sehemu yao ya kusaidia uwanda huu. Pamoja
na changamoto hizo,Farida alisema anamatumaini katika ukuaji wa filamu
za Bongo.
Mjadala
huo ulihudhuriwa na watengenezaji wa filamu kutoka Rwanda, Afrika
Kusini, Nigeria, Namibia, Kenya, Marekani, Sweden na wasanii wa filamu
za Bongo.
Zuku
ambayo ni kampuni ya TV ya kulipia ambayo inaendelea kukua kwa kasi
inapatikana Tanzania, Uganda na Kenya, ina nia ya kudhamini ZiFF kwa
kipindi cha miaka 10 kwa thamani ya jumla ya dola milioni moja.
Udhamini
huo unatarajiwa kutoa utulivu na msaada ambayo kwa upande utachangia
kwa kiasi kikubwa katika kuboresha sekta ya filamu, si tu nchini
Tanzania lakini maeneo mengine ya Afrika.
Kingamuzi
cha Zuku kinatoa wigo mpana wa uchaguzi wa burudani ka vile habari za
michezo, sinema, makala na muziki. Hizi ni pamoja na chaneli tatu za
BBC World News, MTV Base, Setanta Sports, Fox Entertainment na E!. Zuku
pia inatoa chanelli zingine kama Zuku AFrika, Zuku Life, Zuku Sports na
Zuku Movies. Huduma hii patikana kupitia satellite mahali popote
Tanzania
Post a Comment