Na
mwandishi wetu:
KIONGOZI
wa zamani wa bendi ya Diamond Sound ‘Dar es Salaam Kibinda Nkoi’, Ibonga
Katumbi ‘Jesus’ mwezi ujao ataungana na baadhi ya wanamuziki wengine wa kundi
hilo katika onyesho la Usiku wa Sauti na Marafiki wa Kweli litakalofanyika
katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.
Akizungumza
mjini Dar es Salaam jana, mratibu wa tamasha hilo Martin Kadinda ‘Single
Button’ alisema onyesho hilo linahusisha wanamuziki wakongwe ambao wataungana
na Jesus pamoja hao wa Diamond.
“Kila
kitu kinaenda sawa aliyekuwa amealikwa kwenye onyesho ni Jesus lakini katika
onyesho hilo atatakiwa kuimba nyimbo zake kadhaa ambazo alitamba nazo akiwa
Diamond na Beta Musica kwa hali hiyo alishauri aite wenzake ili wamsindikize.
“
Kutokana na heshima walijengeana wenzake walikubali kumsindikiza, kwa hiyo
mashabiki wa Kibinda Nkoi baada ya miaka 12 wataweza kuwaona tena Ibonga
Katumbi, Richard Mangustino, Wayne Zola Ndonga na Alain Mulumba Kashama
wakisimama pamoja na kuimba tena nyimbo zao kali,” alisema Kadinda.
Kadinda
alisema lengo kubwa la onyesho hilo ni kuthamini muziki wa zamani na kufundisha
matumizi ya vyombo vya muziki.
Katika
onyesho hilo pia watakuwepo wapiga magitaa kama Elly Chinyama, Adolph Mbinga,
Marcis Mengi na mpiga drum wa mwisho kuipigia Diamond Sound Kata Nyama
Serikali.
Baadhi ya nyimbo
zitakazopigwa katika onyesho hilo ni pamoja na Neema, Mugheni, Chance, Jetou,
Bana Beta, Midabwada na Infarouge.
Kadinda alisema wanamuzki wengine watakaoshiriki kwenye onyesho hilo
wataendelea kutangazwa.
Post a Comment