Redsan |
Msanii wa nchini Kenya Swabri Mohammed
maarufu kama Redsan amesema alikataa deal la kupiga picha za utupu kwa sababu
hiyo sio tabia yake.
Katika interview aliyofanya na mtangazaji
wa radio moja nchini Kenya aitwae Adelle ambae alikuwa anamuuliza kuhusu maisha
yake, mtangazaji huyo alimuuliza Redsan kama alishawahi kupiga picha akiwa
naked, na jibu la Redsan liliambatana na taarifa ambayo iliwashtua mashabiki
wengi.
“Nakutaka” hit maker alisema hajawahi
kupiga picha akiwa mtupu na hatafanya hivyo, kaisha akaongeza kuwa “actually hivi
karibuni jarida la Fitness walipropose nipige picha nikiwa bila nguo, lakini
nikawaambia hiyo sio style yangu.”
Watu
maarufu wengi hasa waimbaji na wasanii
wa kuigiza wamekuwa wakipiga picha zinazoonesha wakiwa nusu uchi ama
hata wako
naked, kutokana na kuwa siku za karibuni Kenya kumekuwepo na baadhi ya
majarida yanayotoa mpunga mrefu kwa ajili ya matangazo ya picha za
aina hiyo. Tunaweza kusema kwa kulingana na maadili ya kiafrika basi
Redsan ni
mfano wa kuigwa.
Mwanzoni mwa mwaka huu media zilimuandama
sana Redsan baada ya kufungwa minyororo ya mapenzi na msichana aliyemaliza chuo
Kikuu cha Nairobi Viverz a.k.a Lilo ambae alituhumiwa kumpiga limbwata , ‘juju’
ama Kamote kama inavyojulikana huko Kenya ili amuibe kutoka kwa girlfriend wake
aliyejulikana kwa jina la Delilah.
Rumors zilizozagaa kwenye mitaa ya Nairobi
zilisema mwanadada Lilo alizuga anaujauzito ili kumkoleza zaidi Redsan, na
Redsan akachukua jukumu lote na inasemekana walifunga ndoa ya kwa usiri maeneo ya Pangani.
Post a Comment