Kamanda
wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Charles Kenyela amethibitisha
jeshi lake kumshikilia msanii Lord Eyes ambae toka weekend iliyopita
taarifa zake zimesambaa baada ya kushutumiwa kuhusika na wizi wa vifaa
mbalimbali kwenye gari la mwimbaji Ommy Dimpoz.
Namkariri
Charles Kenyela akisema “ni kweli Isaac Waziri Maputo mwenye umri wa
miaka 28 alikamatwa tarehe 20 mwezi wa kumi usiku maeneo ya Kinondoni,
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu ni kutokana na taarifa tulizozipata kupitia
kwa binti mmoja aitwae Kurushinde Hillary (22) mwenye asili ya
kiburushi lakini mkazi wa Mwananyamala kwa Makoma Dar es salaam,
alikamatwa siku hiyo hiyo kabla ya Lord Eyes”
“Alikamatwa
kuhusiana na matukio ya wizi kwenye magari yani kuna mtindo ambao
umeibuka ambapo ukipaki gari yako gari nyingine ya wezi inakuja inapaki
jirani na gari yako ambapo kwa muda mfupi wanafanya utundu wao
wanaoujua, wanafungua gari na kuiba mali iliyoko ndani, mara baada ya
huyu binti kukamatwa katika kuhojiwa mtandao wake anaoshirikiana nao
alimtaja mtuhumiwa Isaac Waziri Maputo (Lord Eyes)” – Kamanda Kenyela
Kwenye
sentensi nyingine Kamanda Kenyela amesema “watu wengi wamelalamika
kuibiwa laptop zao, mabegi, mifuko na hata silaha kwa maana mtu anakua
anajiamini anaacha kwenye gari akiamini kwamba ameshalock lakini watu
hawa na mtandao wao wamekua ni hatari kiasi kwamba wameliza watu wengi”
“Watuhumiwa
hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes tunawashikilia kwa tuhuma zipatazo
30, yani matukio mbalimbali 30 pengine yanaweza yakaongezeka ambayo
yameripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali kama vile Mlimani City,
Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama Coco beach, kwenye kumbi mbalimbali
za starehe na pia kwenye maeneo ambayo kunakua na harusi, sehemu ambazo
kunakua na magari mengi watu hawa ndio huwa wanaitumia hiyo nafasi
kufanya uhalifu, tunawashikilia kwa makosa ya wizi”
KUHUSIANA NA TUHUMA ZA WIZI ZINAZOMKABILI MSANII LORD EYES LIMEPOKELEWA TOFAUTI TOFAUTI NA WASANII WENZAKE:
1:C PWAA ameandika jana kupitia ACC yake ya FB ,akishauri WASANII hao wawili kusameheana,kwa mkosaji kukubali kosa kama amehusika na mkosewa kusamehe kwa masharti nafuu ili AMANI iweze kutawala.
2-RAMA DEE Leo ameandika kupitia kurasa yake ya FB KWA MAWAZO tofa
uti
kidogo kwa kuanza kumkandia LORD EYES kwa kuendekeza tabia zake za
uvutaji madawa ya kulevya:LORD EYES uwe umeiba ama hujaiba kutokana na
tabia za utumiaji MADAWA YA KULEVYA,lazima utahusishwa na mambo kama
hayo ya wizi,nakuongeza"MCHIZI GARI LIMEWAKA ANAHITAJI MSAADA,HALI YAKE
NI MBAYA,Pia kwa ANGALIZO RAMA DEE anasema kama ushahidi utadhihirisha
LORD hajaiba OMMY DIMPOZ juwa SHOW zake zitaishia CHALINZE Pale ARUSHA
baadae sana.
OMMY DIMPOZ naye ameandika kupitia ukurasa wake wa TWITTER leo akidai kinachomuuma LORD EYES alidhamiria coz GARI yangu anaijuwa na MIZINGA huwa akinipiga huwa namtoa...
Msemaji
wa kundi la Weusi Nikki wa Pili ametoa kauli ya kwanza toka kukamatwa
kwa Lord Eyez wa kundi hilo kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy
Dimpoz.
Namkariri
Nikki wa Pili akisema “kwanza hiyo ni habari ya ghafla alafu ni ya
kusikitisha na kushtua, ni habari ambayo imetupa shida na mpaka sasa
inatupa shida sana kwa sababu watu wengi wanatupigia simu kutuuliza
inakuaje”
“Ukiangalia
kwenye mitandao ya facebook na twitter kote imesambaa, unajua ukijua
ukweli ni kitu cha msingi sana kwa sababu sisi pia tulikua hatufahamu
kilichotokea, kwa hiyo cha kwanza tulichokifanya ni kutaka kujua
kilichotokea, mfano mimi niliona kwenye mitandao kwamba Lord Eyes
amekamatwa kwenye eneo la tukio yupo kwenye gari lakini kufatilia nikaja
kugundua haikua eneo la tukio na sio gari hilo, uhalifu ulifanyika
alhamis na alikamatwa jumamosi” – Nikki wa Pili
“Kitu
cha busara tulichoamua kufanya tumeamua kufatilia kisheria ili tujue
uhalisia ni upi ili tuweze kutoa tamko kwa sababu sisi wenyewe Lord Eyez
hatujamuona wala hatujaongea nae, na kingine ambacho kinasikitisha ni
kwamba Lord Eyez ndio ametuhumiwa kama mtu binafsi lakini ukiangalia
kwenye mitandao watu wanawashambulia weusi kitu ambacho sio sahihi
kabisa, mimi Joh Makini, Bonta, G Nako tumepokea hiyo habari kama mtu
mwingine yeyote” – Nikki wa Pili.
duuuh WHAT REAL SITUATION-POLICE WE NEED 2 KNOW DA TRUTH.....
Post a Comment