MSANII
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ney wa Mitego, yupo kwenye hatihati
ya kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) baada ya kuachia remix
ya wimbo wake wa Nasema Nao iliyojaa matusi na maneno makali dhidi ya
wasanii wenzake na watu mbalimbali, Showbiz inakujuza.
Kwa
mujibu wa afisa mmoja wa Basata aliyeomba hifadhi ya jina lake kwani si
msemaji rasmi, katika wimbo huo ulioanza kusikika mwishoni mwa wiki
iliyopita, Ney wa Mitego ametumia lugha ya matusi na maneno yasiyo ya
kistaarabu, huku akiwataja kwa majina watu aliowalenga, jambo ambalo ni
kinyume na sheria za baraza hilo.
Baada ya kupata nyepesi hizo kutoka Basata, Showbiz ilimtafuta Ney
wa Mitego ambaye alisema kuwa wimbo huo wa Nasema Nao Remix umevujishwa
na watu asiowatambua bila idhini yake lakini akaeleza kuwa hajapokea
taarifa yoyote kutoka Basata juu ya kufungiwa.
Post a Comment