Producer mkongwe ambae alitisha miaka flani na ngoma
alizofanya kama 'Fid Q.com' na 'Usiulize' anayejulikana kama Baucha wa Baucha
Records ameelezea vitu ambavyo vimebadilika hivi sasa katika game hasa kwa
upande wa utayarishaji wa muziki ukilinganisha na enzi zile walipokuwa wao ndo
wana-run the game.
katika interview aliyofanya hivi karibuni na josefly wa radio
victoria fm ya Musoma, Baucha alifunguka kuwa kati ya vitu ambavyo anaona
havikuwa sawa na hadi sasa haviko sawa katika tasnia ya utayarishaji ni kwamba
baadhi ya watu walikuwa wanaingia tu kwenye tasnia hii bila hata kupata elimu
hasa ambayo itawasaidia kufanya kazi kwa kiwango kinachostahili. Lakini pia
Serikali haikuwa na sapoti na kuutambua muziki kama biashara, ila ilikuwa
inajulikana kama sehemu ya burudani tu,
Alipoulizwa sababu maoni yake kwa watayarishaji wa muziki
ambao wanajifunza kwa kutumia utundu wao tu lakini hawakusomea maswala ya
utayarishaji wa muziki.
"Nawashauri kwamba tuingie sana kwa sababu tasnia ya
sanaa sasa hivi lazima na elimu iwemo, lazima tuwe na elimu, sasa kwa wale
ambao hawakusoma labda sasa hizi waingie kwenye kusoma ili tuweze kuitoa sanaa
zaidi kutoka kwenye nchi hii kuipeleka kuipeleka kimataifa zaidi, hilo ndilo
swala la msingi sana," alifunguka Baucha.
Baucha ambae alikuwa kimya lakini hivi karibuni amerudi kwa
kishindo na ngoma yake kali akiwa na Ali Kiba "Kelele" amesema sasa
amerudi rasmi kwenye game na yupo0 kivyote kuanzia utayarishaji wa muziki, na
uimbaji, na kwamba anampango wa kuzunguka mikoani ili kuibua vipaji ambapo
atarekodi kazi za wasanii ambao anaona wanafaa.
Kwa sasa Baucha yuko Paris Ufaransa kuangalia kwa lengo la
kuangalia vifaa vya studio, kisha ataelekea Sweden kwa ajili ya show ya mkesha
wa mwaka mpya, pia ataelekea pia Berlin Ujeruman ambako atakutana na Snaa lee
ambae zamani aliitwa Snop Lee, na Baucha amepanga kufanya nae wimbo.
kwa mujibu wa Baucha
mwenyewe kupitia ukurasa wake wa facebook amesema anatarajia kurudi Tanzania
January 8 kwa ajili ya kuendelea na kazi zenye ubora zaidi ndani ya studio yake
(Baucha Records).
All the best Baucha tunatarajia mengi mazuri na makubwa kwa
wadau wa muziki kama wewe kwa ajili ya kuinua mziki wetu wa Tanzania zaidi.
Post a Comment