Wengi waliousikia wimbo wa Roma wa 2030 walipata hisia kuwa
kulikuwa na punch kwa A.City artists Over Tanga ambapo ndo sehemu anakotokea,
ama waliposikia mistari kwenye mashairi ya wimbo wake mmoja akisema 'Hip Hop
ina uwanja mpana usiseme tu iko R-Chuga'. Kama wewe ni mmoja wao utakuwa
unakosea hivi na inabidi umsome tena Roma.
Hivi ndivyo alivyosema Roma kupitia ukurasa wake wa facebook
na kuambatanisha na picha akiwa na Mo Plus na Banx Baba la Ukoo.
"KILA NIENDAPO ARUSHA (ARACHUGA)!!! HUPENDA KUFANYA
NGOMA NA MANINJA WA KULE!! DX HUSIMAMIA MIZIGO YOTE HII
with ma ninja BAAAANXXXX na MO PLUS BABA LA UKOO
NGOMA INAITWA "UKWELI"
A.city "
R.O.M.A (Rhymes Of Magic Atraction) ndivyo anavyojiita na
kulitafsiri jina lake, kila akitoa wimbo mashairi yake huwa na nguvu ya ajabu
kuvuta attention ya wasikilizaji wake kitu ambacho kimesababisha watu wengi
kuvutika na kununua wimbo wake 2030 kwa shillingi 3000 kwa njia ya email,
lakini pia baada ya kuuachia tu uliongoza kwa kupakuliwa kwenye mtandao kwa
hapa Tanzania.
Post a Comment