Unajua Stamina alipanga kufanya nini na Kanumba & Sharo Milionea? Asema mwaka 2013 'tutaoneshana ubaya', azungumzia pia sababu za Mtu Chee kuzima kwa muda.


Mkali wa michano aliyetisha sana mwaka 2012 Stamina a.k.a Kabwela amefunguka kuhusu mipango mbalimbali aliyokuwa nayo mwaka jana na hatua aliyopiga katika muziki wake na show 61 alizopiga mwaka huo. Kuhusu show alizopiga mwaka jana show ambayo hataisahau ni show ya Fiesta Dar ambayo alifunika vibaya na kwamba hakuwahi kufanya show kama ile.

'Kabwela' hitmaker mwenye misemo kama kamusi amefunguka katika interview aliyofanya na Lucas Maziku wa Radio SAUT Fm ya Mwanza, kuwa mwaka 2012 alipanga kufanya kazi na marehemu Steven Kanumba, na walipanga kufanya movie ya wimbo wake wa "Kabwela" lakini bahati mbaya alifariki kabla hawajakamilisha mpango wao huo, lakini mwaka huu ataifanya movie hiyo.
Lakini pia Marehemu Sharomilionea alipanga kumpa shavu kwenye wimbo wake mmoja ambao Sharo alipanga kumuimbia mama yake, na mipango ilikuwa tayari lakini Sharo alisema itabidi asafiri akirudi watafanya wimbo huo pale C9, na bahati mbaya hakurudi baada baada ya kupata ajali na kufariki.
 "Hata kwenye ule wimbo tulifanya wa kumuenzi nilisema, alisema kwamba akisafiri akirudi, kuna ngoma tutafanya alikuwa anamuimbia mama yake, nikikuwa mimi niko featured, alilkuwa kanishirikisha, ikuwa inataka kufanyika pale kwa C9 lakini na yenyewe pia Mungu kampenda zaidi, kwa hiyo ni vitu ambavyo vinaniuma sana."
Kuhusu mafanikio aliyoyapata ni kwamba alifikia level nzuri sana alihama kutoka kwao na kupanga ili aishi maisha yake mwenyewe, hakuwa na uwezo wa kwenda chuo kwa sababu ya mkwanja lakini sasa hivi ameshakichanga na yuko tayari kuingia chuo mwaka huu. Akicheka kwa kwa utani kidogo alisema hadi sasa anafurahi kuona anaendesha gari lake mwenyewe.
Stamina amesema ameweza pia kuzifikia sehemu ya ndoto yake, na kwamba ameweza kufanya kazi na msanii anaemkubali sana Fareed Kubanda a.k.a Fid Q, na kwamba amefanya nae ngoma yake mpya inayoitwa "Toleo Jipya". Sio hayo tu lakini pia ngoma imefanywa kwa producer of his dream P-Funky Majani.
Kuhusu Kutosikika kwa muda kwa kundi la Mtu Chee linaloundwa na yeye, Country Boy na Young D, amesema mgao wa mapato ulileta shida ukizingatia wao hawakuwa na meneja na Young D ana management yake tayari, meneja wa Young D alikuwa anataka asilimia nyingi zaidi ya mgao na sio mgao ulio sawa kwa member wote kitu ambacho kilileta utata na kulinyamazisha kwa muda kundi hilo, lakini sasa wameshakubaliana na management ya Young D na wanarudi tena hewani kama Mtu Chee.
Pamoja na mafanikio aliyoyapata mwaka jana, bado Stamina anaona kama haijawa poa kiivyo na mwaka huu ndio utakuwa mwaka wa kuoneshana ubaya.
 "Nahisi kama mwaka 2012 sikufanya kitu lakini mwaka 2013 ndo tutaoneshana ubaya, kwa sababu kuna project nyingi sana zinakuja ukiacha mbali hiyo ngoma yangu na Fid, video yake...halafu mwisho wa mwezi wa kwanza ntadrop album yangu ya kwanza uswahilini, iko tayari inaitwa "ALISEMA".
Stamina amesema ameshafanya kazi na msanii toka Kenya Colo, na sasa anafanya mpango wa kufanya kazi na Keko wa Uganda, na yote hayo anamshukuru fan wake aliyempa nafasi na sapoti ya kufika hapo alipo. Nice move Stamina endelea kukimbia na tunakutakia kila la-kheri mwaka huu.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates