Home
»Unlabelled
» MAKOSA SABA 7 NEY WA MITEGO NA DIAMOND WALIVYOIKOSEA HIP HOP.
MAKOSA SABA 7 NEY WA MITEGO NA DIAMOND WALIVYOIKOSEA HIP HOP.
By
Unknown
•
12:59 PM
•
•
MAKOSA SABA 7 NEY WA MITEGO NA DIAMOND WALIVYOIKOSEA HIP HOP.
MAMBO VIPI?,NATUMAI NI WAZIMA WA AFYA TELE.KARIBUNI TENA KATIKA MAKALA
YA TATU KATIKA KITIVO CHA RAP.MIEZI KADHAA ILIYOPITA NILIPATA KUSIKILIZA
KIBAO CHA MSANII NEY WA MITEGO ALICHOMSHIRIKISHA MWIMBAJI AITWAYE
DIAMOND.KIBAO HICHO KINAFAHAMIKA KAMA "MUZIKI GANI". NIMESHAWISHIKA
KUCHAMBUA KIBAO HIKI KWA SABABU KUU MOJA.SABABU HIYO NI KWAMBA
KINACHOZUNGUMZIWA NI HIP HOP NA SIO KWASABABU UMEFANYWA NA NEY WA MITEGO
NA DIAMOND.
KATIKA KIBAO HIKI NILIPATA KUSIKILIZA NA KUGUNDUA
BAADHI YA MAMBO AMBAYO HAYAJAUTENDEA HAKI UTAMADUNI WA HIP HOP AMBAYO
YANANIFANYA KUSHAWISHIKA KUSEMA WAHUSIKA WALIOHUSIKA KUFANYA KIBAO HIKI
WAMEUKOSEA UTAMADUNI WA HIP HOP.
YAFUATAYO NI MAKOSA SABA YALIYOFANYWA NA WAHUSIKA WA KIBAO HIKI.
(1) MC HAIMBI,MC ANACHANA.KOSA HILI LIMEFANYWA NA DIAMOND KATIKA KIBWAGIZO
CHA WIMBO HUU ANAPOSEMA ''HIVI NYIE MA EMCEE MNACHOIMBA KITU GANI..''.
JAPO KUWA MC LAZIMA UJUE KUCHANA PEKEE HAKUKUFANYI KUWA MC WA HIP HOP
LAZIMA UJUE MISINGI YA HIP HOP PIA.
(2) KUJUMUISHA TABIA ZA WATU BINAFSI KATIKA UTAMADUNI WA HIP HOP."
MHUSIKA (DIAMOND) AMESHINDWA KUTOFAUTISHA KWAMBA KUNA TABIA BINAFSI ZA
MTU KAMA UBABE/UGOMVI,ULEVI,MATUSI N.K..HILI LINAFANYIKA PALE ANAPOSEMA
"NYIE WATEMI MTAANZISHA UTATA,MICHEZO YENU KUTOBOA PUA...'' NA "MARA
BANGI MARA MATUSI SANA".
HAKUNA MAHALI KATIKA UTAMADUNI WA HIP HOP
TUNAAMBIWA TUFANYE HIVYO NDIO MAANA KIKOSI CHA MIZINGA WANA KIBAO CHAO
KINAITWA "HIP HOP BILA MADAWA INAWEZEKANA".
(3) "KUCHANGANYA VINA VYA HIP HOP NA VINA VYA MALENGA''.
KATIKA KIBAO HIKI NEY WA MITEGO HAJAITENDEA HAKI HIP HOP PALE MISTARI
YAKE INAPOKOSA VINA VYA HIP HOP.VINA KATIKA HIP HOP NI ULE MFANANO AU
MSHABIHIANO WA SAUTI MBILI BAINA YA MISTARI MIWILI NA KUENDELEA
MFANO;KISIMA - MLIMA.ILA VINA VYA MALENGA HUEGEMEA KATIKA UFANANO WA
SAUTI MOJA YA MWISHO AU SILABI YA MWISHO MFANO;MKITO - MVUTO NEY WA
MITEGO ANACHANGANYA PALE ANAPOSEMA ''HAMJANISHAWISHI BONGO FLEVA INANIPA
KICHEFUCHEFU/KWANZA NYIE MALIMBUKENI WA UMAARUFU/'' N.K
(4) "KUKOSA VINA KABISA''
KWENYE UBETI WA PILI MWANZONI NEY WA MITEGO ANAKOSA VINA KABISA HATA
VYA MALENGA ANAPOSEMA "MZIKI WENU USHIRIKINA NDIO UMETAWALA/Q CHILLA
ANALALAMA ANSEMA UMEMROGA/MGANGA ALIYEKUTOA UMEMKIMBIA HUJAMLIPA/BILA
SKENDO ZA MAGAZETI BASI HUSKIKI/".
(5) "HIP HOP INAHUSIKA NA MAPENZI PIA''
UTAMADUNI WA HIP HOP UNAGUSA NYANJA ZOTE ZA MAISHA,KISIASA,KIUCHUMI,KIUTAMADUNI NA KIJAMII AMBAMO KUNA MAPENZI NDANI YAKE.KOSA HILI ANAFANYA NEY WA MITEGO ANAPOSEMA ''TUSHACHOSHWA KUTOA MAPENZI...''
(6) ''WANA HIP HOP WANAFANYA WASICHOKIJUA''
DIAMOND ANASEMA ''BADILIKA USIWE MJINGA... MJINGA AU IGNORANT
(KIINGEREZA) NI MTU AMBAYE AMEKOSA MAARIFA/UFAHAMU AU KUTOKUJUA
KITU/JAMBO FULANI.DIAMOND ANAMAANISHA WANA HIP HOP WANAFANYA
WASICHOKIJUA KWA SABABU WANAFANYA BILA MAARIFA NA UFAHAMU KITU AMBACHO
SI SAHIHI.
(7) ''MDUNDO SIO WA HIP HOP''
HAIWEZEKANI KUITETEA
HIP HOP KATIKA MDUNDO HAUNA VIONJO/LADHA YA HIP HOP.NEY WA MITEGO
HAJAITENDEA HAKI HIP HOP ALIYOKUWA ANAITETEA.
SIMILAR ARTICLES
Post a Comment