Home
»Unlabelled
» MASOGANGE NA MWENZAKE YAMEWAKUTA HUKO AFRIKA YA KUSINI
MASOGANGE NA MWENZAKE YAMEWAKUTA HUKO AFRIKA YA KUSINI
By
Unknown
•
10:55 AM
•
•
HATIMAYE wale Wanawake wawili walionaswa na madawa ya kulevya
Afrika kusini wametambuliwa kuwa ni mabinti wa KITANZANIA ..
Mabinti hao wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za
kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini
wakitokea Tanzania.
Akizungumza na mwandishi wetu jana, Kamanda wa
Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa,
alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald
(MASOGANGE) ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa
mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye
alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24.
Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.
Amesema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea
kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia
linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Jumapili
iliyopita mtandao huu ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya
aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini
wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la
Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.
Wanawake
hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa
na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150
za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya
bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.
Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao
walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la
dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.
Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza
katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na
kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799
walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.
Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa
katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu
taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu
na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.
Pinda
alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya
katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.
Alisema
vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata
sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na
kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani
SIMILAR ARTICLES
Post a Comment