Paka mwenye jina Marsik wa Urusi amesafirishwa na ndege binafsi ya
Paramount Business Jets (PBJ), kutoka Urusi hadi Marekani kwa gharama ya
dola laki moja ambazo ni sawa na shilingi milioni 162 za Tanzania.
Akisafiri kutoka Urusi hadi Marekani, Marsik anadaiwa kupata huduma ya nguvu kabla hajapanda na ndani ya ndege hiyo.
Vyeti vyake vya afya vinavyoonesha chanjo alizopata alivipata saa 24 kabla ya safari kuanza.
Tajiri huyo anadai kutumia kiasi chote hicho ili kuhakikisha kuwa paka
wake anafika Marekani salama na kuepuka kunyanyasika ama kifo kwakuwa
baadhi ya wanyama wanaosafiri kwa ndege za kawaida huwekwa kwenye sehemu
ya mizigo hupoteza maisha.
Source: prweb.com
Post a Comment