SEHEMU YA KWANZA
Jua kali la saa 9 lilikuwa linawaka kupita
maelezo, Rashid ni kijana mwenye uchu wa maendeleo alipenda kujituma kama
mtumwa akiwa na lengo la kuishi kama mfalme, wakati huu Rashid alikuwa
kibaruani maeneo ya Raha leo pale linapojengwa ghorofa, hapa palikuwa na
mchanganyiko wa wanaume na wanawake watoto na watu wazima palikuwa na
wakandarasi kutoka India na Tanzania Bara, kila mtu alikuwa akisghulika kufanya kazi aliyopangiwa lakini bado
kulikuwa na unyanyasaji kutoka kwa wasimamizi wao.
“Wewe mpumbavu tena
mzembe kabisa masaa mawili unachanganya mchanga uwo kama umeshindwa kazi ni
bora useme mjinga wewe kuna watu kibao ambao wanatafuta kazi wewe umepata
unaizembea nasema kama huwezi kazi nenda kapakatane na mzee walo nyumbani..” Rashid alitolewa maneno makali
yaliochangayika na matusi ya nguoni.
Lakini bosi……. Rashid
alijaribu kujitetea lakini hafla alikatishwa na bos wake “lakini kitu gani tena hakuna malipo leo mana sjaona la mana ulofanya
tangu asubuhi.” Yule msimamizi aliyekuwa akisimamia kundi la akina Rashid
aliondoka huku akionesha ni mwenye hasira na kumuacha Rashid akiwa ameduwaa.
Ilivyofika saa kumi na mbili za jioni ulikuwa
mda wa malipo kwa wafanya kazi walikuwa wamejinga mstari mmjoa ulio kuwa mrefu.
“Ipo kuja haraka
nasubiri nini hapa …” Muhindi alikuwa akimuhimiza moja wa kibarua ambae imefika zamu yake
kwenda juchukua malipo, aliangalia jina lake na kusema ok nimeona jina yako nalipa elfu nne ….. waliendelea kwa mfumo
uleule hadi zamu ya Rashid imefika sema haraka naitwa nani? Muhindi
alimuharakiza Rashid ambae alionekana kama amechoka kutokana na kazi aliofanya “Rashid ..Rashid naitwa ….” Rashid
alijibu haraka haraka na Yule Muhind alikuwa akiangalia kwa makini lakini
hakuliona jina la Rashid “wewe mbona
natania mimi hapana ona jina la Rashid mimi ipo nafanya mchezo sio pisha
nyengne apaa”… Rashid aliduwa na kutojua nini cha kufanya, ilimlazimu
aandoke maeneo ya pale na kuelekea Daraja bovu kwani ndipo alipokuwa anakaa.
Wakati huu
ilikuwa magharibi imeshaingia akapita njia ya Kwahaji tumbo na kuitafuta
Makadara huku akiwa amechoka,Rashid alikuwa mrefu kiasi na sio mpana sana pia
mweusi kiasi kwa upande wa ngozi yake ya mwili hapa alikuwa amevaa pensi ya kak
iliyochafuka kwa saruji pia alikua juu alikuwa amevaa shart nyeusi pia
inaonekana kama imechakaa, wakiti alipokuwa njiani hakuwa akikazana kwani
alionekana kama amechoka pia mwenye mawazo baadhi ya mda alikuwa kama akiongeqa
peke yako na kujishtukia wakati anapo pishana na watu.
Kitu
kilichokuwa kimfariji njiani na kusahau yale yalotekea pale Rahaleo na kumpa
nguvu ya kutembea ni Radio ambazo alikuwa anaziskia njiani haswa ambazo
zilikuwa na program za music alikua akizifuatishia kila nyimbo anayosikia
alikua akipata hasira kila anaposikia nyimbo iliyokuwa haina kiwango kizuri kwani yeye kuhangaika kote
huko kulikua ni kutafatuta pesa ya kwenda studio na wakati mwengine alikua akihisi kama
anafanyiwa interview kwenye radio kumbe
anajiuliza maswali mwenyewe na kujijibu.
………………………..
Shikamoo mama.. Rashid alimsalimia
mama yake aliyekuwa amekaa barazani. “Marhaba!
Za uko utokapo?” Bi Key mama yake
na Rashid alimuitikia salamu, “Salama tu
mama vipi chakula tayari mana nina njaa hatari mama kazi leo ilikuwa ngumu.” Rashid
alilalama kwa mama yake. Mwanangu riski
imepatikana hivi jioni nimeuza ule mkoba wa ukili tena pesa nimepewa nusu
nasubir maji yapate moto nikabandike ugali subiri kidogo.” Bi key alimjibu
Rashidi lakini Rashid hakuonesha kufurahia na majibu aliyopewa kutoka na njaa
iliyokuwaikimparama alihisi kama tumboni kuna simba anamparura na makucha yake,
aliingia ndani akiwa na mawazo ya kuenda kuoga. “Aghaaa shit”, Rashid alisema huku akizipiga mateke ndoo za maji
mana zilionekana zikiwa tupu ikabidi achukuwe na kwenda mferejini kuenda
kutafuta maji,
Wakati alipofika mferejini alikuta umati w
watu wakisubiri maji ikamlazimu akae foleni, mara alitokea Yahya rafiki yakme
na Rashidi ambae alionekana akiwa mardadi alivaa shati ya rangi nyeupe na
suruali aina ya jeans rangi nyeupe pia chini alivaa raba aina ya All star na mkononi
alikuwa na saa aina ya Lacoste. Vipi
Chidi! Yahya alimsalimia rafiki yake
Rashid ambae mara nyingi alipenda kumuita kwa kumkatisha jina na kumita Chidi.
"poa inakuaje chif?" Rashid
alimuitikia salamu Yahya na kumbambika suala "vipi naona umetokelezea wapi tena? Yahya alitabasamu na kumjibu
Rashidi "ahh wapi kawaida tu naenda
kwa shemegi yako Latifa si unajua tena...." Dah nakukubali kaka vipi Najma
kwani au ndo ushapotea? Rashid alimuliza suala Yahya huku akionesha
tabasamu na kujawa hamu ya kutaka kujua. Yahya alimjibu kwa mbwembwe nyingi
Rashid "wewe vipi Najma ndo mwanamke
wa malengo yangu hawa wengine nazingua tu kutoa baridi mwilini" Rashid alicheka kwa kicheko kisicho na
kawaida hadi watu wote pale mferejini wakawa wana jiuliza kulikoni, mara simu
ya Yahya iliita "Oyo sasa me nasepa namuwahi huyu mana do
ananiharakiza kama vipi nitgakutafuta mana nimesikia tangazo redio kuwa
wanatafuta vipaji vipi umesikiaa" Rashid alionekana kuduwaa "hapana
sijasikiaa....."
USIKOSE
KUFATILIA SEHEMU YA PILI
Post a Comment