Pamoja na mchezo wa watani wa jadi kuisha kwa sare ya 3-3
Jumapili ya wiki iliyopita, Simba wameanza kuongoza katika kampeni ya
"Nani Mtani Jembe?" inayoendelea hivi sasa kwa kuwashirikisha
mashabiki wa klabu hizi mbili kongwe nchini.
Mpaka sasa Simba wana kitita cha Shilingi
50,012,500.00 wakati watani wao wa jadi Yanga wana Shilingi 49,987,500.00.
Upigaji wa kura katika kampeni hii unahusisha mashabiki kununua Bia ya
Kilimanjaro na kusoma namba zilizo chini ya kizibo na kutuma kwa ujumbe wa simu
wakianza na jina la timu wanayoishabikia kwenda 15440 na moja kwa moja Shilingi
1,000 kupunguzwa kutoka kwa wapinzani na kuwekwa kwa timu yao. Matokeo ya Nani
Mtani Jembe yanapatikana katika tovuti ya http://kilitime.co.tz/campaigns/nmj/
Post a Comment