Home
»Unlabelled
» TAHADHARI : USIKUBALI KUTAPELIWA :
TAHADHARI : USIKUBALI KUTAPELIWA :
By
Unknown
•
8:58 AM
•
•
Inazidi kudhihirika kuwa ANTHONY SHILLIYE LUCAS ambaye anadai kuwa ni
Mhasibu wa kampuni inayoitwa SOCIAL CREDIT COMPANY ni TAPELI na MWIZI WA
MTANDAO.
Hadi sasa amewatapeli watu wengi kwa kuwataka
wamtumia fedha kiasi cha shs. 45,000/- kupitia namba ya MPESA 0756 310
988 (ANTHONY SHILLIYE) na TIGOPESA 0714 254 735 (ANTHONY LUCAS).
Mchezo anaofanya kusambaza habari zake za utapeli ni kupitia “INTERNET
PHISING” ambapo anaiba user name na password za akaunti za facebook za
watu mbalimbali na wakati mwingine kutengeneza akaunti feki ambazo
huzitumia kuwashawishi watu kuhusu kuwepo kwa mikopo na kampuni hiyo.
Kwahivi sasa Dar24 hatutoi mikopo na wala hatuijui hiyo kampuni. HIVYO
MNATAHADHARISHWA KUTOKUAMINI UJUMBE WOWOTE WA MIKOPO KWENYE FACEBOOK
ACCOUNT HIZO. Taarifa hizi pia ziko POLISI, TCRA na kwenye Kampuni za
Simu.
Tushirikiane kwa kuwatahadharisha watu zaidi kukwepa mtego huu. Pia usifungue akaunti hii : http://www.socialcompany.wapka.mobi/index.html.
SIMILAR ARTICLES
Post a Comment