David Correy akitumbuiza…
“Waving Flag” ni ngoma iliyotokea kupendwa sana,toka kwa rapper mwenye asili ya Somalia, K’naan, si tu kipindi mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2010 yalipokuwa yakiendelea nchini Afrika Kusini, bali hata mara baada ya mashindano hayo kuisha, mdundo huo uliendelea kufanya vizuri sababu ya vionjo vilivyotumika kuitengeneza…
“Mpaka sasa nimefanikiwa kutimiza ndoto kubwa mbili maishani mwangu, kukutana na mama yangu mzazi pamoja na hii ya kuweza kurekodi nyimbo na kampuni hii ya CocaCola” alisema Correy…Pata ladha ya ngoma iyo hapa chini
Kwa sasa, msanii huyu yupo nchini Kenya amabapo amepata mualiko wa kwenda kutumbuiza kibao hicho, na atakuwa nchini humo kwa muda wa siku tatu…
Coca cola 2014 FIFA World Cup Trophy Tour ikiwa inaendelea, ambapo kwa sasa kombe hilo lipo nchini Kenya, Correy anatarajia kuondoka Ijumaa, Novemba 29 ambapo atalisindikiza kombe hilo nchini Tanzania kama ratiba ya safari ya mzunguko wa kombe hilo inavyosema…Itakuwa ni mara ya tatu kwa kombe hili kutembelea Tanzania, ambapo mara ya mwisho lilitua nchini Novemba,2009 na kupokelewa na raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Post a Comment