Bob Junior atengeneza ‘mshiko’ kwa njia ya harus


Hauhitaji degree ili upate hela nyingi kwenye muziki, ni akili na ubunifu tu. Jana rais wa masharobaro, Bob Junior aka Mr. Chocolate Flava, amefunga ndo kwa style yake na kudhihirisha kuwa, msanii anaweza kuingiza hela kwa mgongo wa harusi. Sio kwa michango ya ndugu by the way, ni kwa mashabiki kwenda kulishuhudia jiko lake na pia kuburudika na show ya nguvu kwa kulipa kiingilio.


Producer huyo aliyemtambulisha Diamond na kumtoa kimuziki, aliamua kuua ndege wawili kwa jiwe moja kwa kuunganisha harusi yake na show yake ya jana ya Bilicanas.
Kwa kiongilio cha shilingi elfu sita tu mlangoni, mashabiki wake waliweza kumshuhudia mke wake aliyemtoa Zanzibar. What a wedding!



Awali kabla ya kurejea Dar, Bob Junior alihakikisha pia anachukua hela za wazanzibar katika show aliyoipiga kujitambulisha ‘ukweni.’
Kwenye show hiyo iliyoitwa, “Nichumu, Nikiss Mwaah Nite” iliyofanyika Ngome Kongwe Zanzibar, watu kibao walijitokeza kumuangalia akikata mauno kama kawaida yake na baadaye kumpandisha mke wake stejini.


Miongoni mwa wasanii waliompa tafu kwenye show hiyo ya Zanzibar ni pamoja na Queen Darleen na Cassim.
 

Wow! That was a sellout show!  Hongera Bob.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates