Ray azindua ‘Sobbing Sound’ kwa kusaidia yatima



Muigizaji maarufu wa nchini Tanzania Raymond Kigosi weekend hii amezindua filamu yake mpya iitwayo Sobbing Sound kwa kuendana na shughuli za kutoa msaada kwa watoto yatima.

Kupitia blog yake Ray ameandika, “Hatimaye mzigo wa Sobbing Sound umeingia mtaani kwa aina yake baada ya kaumua kwenda kuuzindua na watoto yatima wa kituo cha Maunga kilichopo maneno ya Kinondoni studio.”
Amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kuguswa na jinsi watoto yatima wanavyoishi katika mazingira magumu.

Ray akikabidhi misaada
Ray akiwa pamoja na watoto yatima
“Hili ni jukumu la watanzania wote kuanza kuguswa katika hili maana hapa duniani sisi ni wapangaji tu makazi yetu ni kwa Mungu Baba, sasa unapopata kidogo jaribu kuwafikiria na wale waliokuwa na maisha magumu, yani tugawane umasikini.”

Aliongeza kwa kusema, “sikuwa na kikubwa sana ila nimejitolea pale nilipoweza kubarikiwa na Mungu Baba. Unaambiwa kuwa kama hutoweza kushukuru kwa kidogo basi hata ukipata kikubwa pia utakuwa mgumu kumshukuru yule aliyekuwezesha kukupa kipato hicho.”


Filamu ya Sobbing Sound imetoka chini ya kampuni ya Steps Entertainment na ameigiza .

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates