Rapper mwenye swagga za 50 Cent, Godzilla ameukosoa
mfumo wa elimu uliopo nchini ambao anadai hautengenezi wataalam. Kupitia
mtandao wa Facebook, Godzilla ameandika:
Mfumo wa Elimu Tanzania inabidi ubadilishwe. Elimu ndefu
sana na haiko katika kutengeneza wataalam(Experts).
Mfano mtu kasoma hadi darasa la 7 akafeli na mtu
aliyesoma hadi Form6 akafeli wote wanakuwa sawa coz hawaajiliwi #so miaka yote
imepotea bure.
Zamani kulikuwa hadi na la 4 la mkoloni wazee wakifika la
4 wanamaliza sa hivi aje wazee?!
Fanyeni mfumo mzuri wa Elimu ili tuwe na wasomi wengi.
Post a Comment