Mkuu wa jeshi la polisi nchini Uganda, IGP, Kale Kayihura amewaagiza maofisa wa
Tanzania kuirudisha haraka passport ya Jose Chameleone.
Kayihura ametoa amri hiyo alipokutana na Chameleon kwenye
kituo cha polisi cha Muyenga mchana wa leo jijini Kampala.
Amesema maafisa wa hapa nchini wamesema passport ya msanii
huyo ingewasili baadaye leo na kukabisdhiwa kwake mara moja.
Leo Jose Chameleone akiwa na mashabiki wake wameandamana
kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kudai arudishiwe passport hiyo
iliyokuwa ikishikiliwa na Erick Shigongo kwa madai kuwa meneja wake amemtapeli
dola 3500.
Post a Comment