Hate it or Love it: Diamond anapiga hela jamani!




Hivi kuna wiki umeshasikia inapita bila kusikia Diamond amepiga show sehemu? Huyu jamaa anapiga show mfululizo na hatudhani kama anapata hata muda wa kupumzika.
Halafu ukisikia amepiga show sehemu weka akilini kuwa hapo kaingiza si chini ya milioni nane,ndogo sana labda milioni tano. Akitoa gharama ndogo ndogo kama za kuwalipa dancers wake n.k, zinazosalia zote zinaenda kwenye akaunti yake mwanangu!

Akaunti inatuna tu. Na nasikia kijana alivyo mchumi kama mchaga, hata buku anaweza asikupe kudadeki! Kama demu akishoboka kwake akitegemea atapewa good times,asahau tu sababu ain’t nothing like that coz the money is going straight to the bank. Juzi kanunua mkoko mpya, kitu cha Prado ambacho kimemnyofoa kama 70 Tshs Milli! Damn! So hate it or love it this dude got cash!!

Jana tu alikuwa Morogoro kwenye show ya Wajanja ya Vodacom akiwa na Fid Q, Mabeste, Shetah,Ommy Dimples na Ney wa Mitego! Nasikia wameangusha show ya kali sana pande hizo na watu walikuwa nyomi balaa, si unajua show za bure!

Kabla ya jana, yeye na dancers wake wakiwa wametupia dress code ya kufa mtu, wamepiga show ya maana sana pande za Dodoma. And the ladies? Kama unavyoweza kuimagine, walikuwa hawakatiki stejini ili tu kumshuhudia kwa karibu mchizi na wengine hawakuna  soo  kuomba japo busu tu! Dah.

Cheki baadhi ya picha za show zake wiki hii.

'Nishike japo mkono tu jamaani'
'Nichumu baasi'
Mashalaa!
'Unasema!'
Nyomii


Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates