Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan ameiponda bodi ya filamu
nchini kuwa imelala na hivyo kushindwa kufanya kazi yake.
Akichangia hoja bungeni kwenye mjadala wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
amesema zipo filamu nyingi zinazoingia nchini zenye mambo machafu lakini
hazichukuliwi hatua yoyote.
Amesema kuna mtindo umekuwa maarufu sana nchini wa
kuingizwa kwa filamu za ngono zilizotengenezwa nje lakini makava yake yakiwa na
picha za wasanii wa Tanzania.
Post a Comment