Monday, July 16, 2012 Utoaji wa Tunzo, kwa Filam Zilizoshinda katika Tamasha la ZIFF la 15 katika viwanja vya Ngomekongwe.

ay, July 16, 2012

Utoaji wa Tunzo, kwa Filam Zilizoshinda katika Tamasha la ZIFF la 15 katika viwanja vya Ngomekongwe.

 
 MC  Farouk akitowa  utaratibu  wa Usiku wa Utoaji wa Tunzo za ZIFF, uliofanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe Usiku wa jana.    
 Wanafunzi wakisoma Utenzi wa Utoaji wa Tunzo kwa Filam Bora katika Tamasha la ZIFF la 15 

Waziri  wa Habaru Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbaruok, akitowa hutuba  katika sherehe za Ufunganji wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar lilofanyika katika Viwanja vya Ngome Kongwe Forodhani na kuitangaza Zanzibar Kiutalii kupitia Tamasha hilo la 15 la ZIFF.

 Mkurugenzi wa ZIFF akiwatambulisha wafanyakazi wa  Tamasha hilo wote wakiwa ni Wazanzibar waliofanikisha Maonesho ya Tamasha kwa sekta zote katika kipindi chote cha maonesho hayo.
Wafanyakazi wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF, vijana wa Kizanzibar  wakiwasalimia Wananchi waliofika katika sherehe za ufungaji wa Tamasha hilo.    
Mkurugenzi wa Kampuni ya ZUKU, akitowa salamu za Kampuni yake kuweza kufanikisha Udhamini wa Tamasha hilo uliofanywa na Kampuni hiyo.  
Mtayarishaji wa Filam ya UHLANGA kutoka Afrika ya Kusini Ndaaba Ka Ngawane, akitowa shukrani kwa kupata ushindi wa Filam yake na kupata ushindi wa jumla kupitia Filam hiyo
 Mtayarishaji  wa Filam ya LUHANGA kutoka Nchini Afrika ya Kusini akiwa na Vijana wake baada ya kukabidhiwa Tunzo yake, na kuibuka mshindi wa Jumla kwa kukusanya Tunzo nyingi katika Tamasha la mwaka huu la 15, kwa ubora wa kazi yake kupitia Filam hiyo.

Mshindi wa Tunzo ya Filam ya Ruhago kutoka Nchini Rwanda Mbabazi Aime Philbert akitowa shukrani kwa ushiindi wa filam yake baada ya kukabidhiwa tunzo yake. 
 Waheshimiwa wakifuatilia vijana wakisoma Maulid ya Home wakati wa utoaji wa Tunzo za ZIFF.
 Vijana wa Mtaa wa Mtendeni wakisoma Maulid ya Home katika Usiku wa Utoaji wa Tunzo za ZIFF kwa mwaka 2012
 Watayarishaji na Wadhamini wa Tamasha la ZIFF wakipiga picha za kumbukumbu ya Tamasha la 15 wakati wa Vijana wa Maulid ya Home wakisoma katika Jukwaa la ZIFF la Ufungaji.
 
Mtayarishaji wa Filam ya ZAMORA kutoka Zanzibar Shamis Bhanji akifurahiya Tunzo yake baada ya kukabiidhiwa kwa kuwa Filam bora kwa Nchi za Afrika Mashariki.
Mwakilishi wa Kampuni ya ZANLINK akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa Cheti cha kufadhili Tamasha hilo kwa Muda wa Miaka Kumi kutowa huduma ya Internet kwa kipindi chote  cha Tamasha.



Wasanii wa Kikundi cha 6B wakionesha umahiri wao wa kucheza  muziki wa aina yote , wakilishambulia jukwaa katika sherehe za ufungaji wa Tamasha hilo.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates