Sam Saintfeit wa Ubelgiji kuwa kocha mpya wa Yanga

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ethiopia mbelgiji Tom Saintfiet ana asilimia zaidi ya 90 ya kuwa kocha mpya wa Yanga.
Kocha huyo pia alikuwa ameomba kuifundisha timu ya taifa ya Kenya, lakini huenda akaja Yanga kwakuwa amepewa dau kubwa zaidi.
“He applied for the Kenya National Team job, but it would seem Yanga have offered him big bucks,” aliandika kocha mwenye leseni ya level B kutoka UEFA, Tom Legg.
Tom Saintfiet aliyezaliwa tarehe 29 March 1973 alianza kuwa kocha akiwa na miaka 24 na kumfanya kuwa manager mwenye umri mdogo zaidi kwenye soka la Ubelgiji.
 
Kiongozi wa usajili wa Yanga, Seif Ahmed alithibitisha kuwa kocha toka Ubelgiji, Tom Saintfiet ni miongoni mwa wawili wenye nafasi kubwa kutua Jangwani.
Timu alizozifundisha
1997-2001 -    Lower Belgian Divisions
2000       -     F.C. Satelitte Abidjan
2002-2003 -   B71 Sandur
2002-2003  -  Stormvogels Telstar
2003-2004 -   Al-Gharafa Sports Club
2004       -     Qatar U-17
2005-2006 -  BV Cloppenburg
2006-2007 -   FC Emmen (Technical Director)
2008       -     RoPS
2008-2010 -   Namibia
2010       -     Zimbabwe
2010-2011 -   Shabab Al-Ordon
2011       -      Ethiopia

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates