Kitaani
kumeibuka tetesi kwamba wale watoto walioonekana kwenye video mpya ya
Ben Pol inayoitwa MANENO kuwa wale ni watoto wa mtaani. Sasa kutokana na
maswali kuwa mengi nikabidi nimtafute Ben Pol na kumuuliza juu ya hili
na yeye akanijibu hivi...Namnukuu
"Wale
watoto kwanza amewatafuta producer wake Karabani, mimi nilichokifanya
nilimlipa gharama zote za kila kitu, na yeye ndo aliyekwenda kuongea na
wazazi wa wale watoto mnaowaona halafu wale sio watoto wa mtaani wale
wana nyumbani kwao wale na wawili pale ni ndugu so walitengenezwa tu
kidizaini,"
Nikamuuliza
je vipi ulipata nafasi ya kuwaona au kukutana nao maana kwenye ile
video kama umeonekana vipande vichache sana tofauti na video zingine
anaonekana mwanzo mwisho
"Yeah
niliwaona na nikapiga nao story na pia wao walikuwa wanatamani kuniona,
na siku moja tulishoot wote, kama video ukiitizama pale darajani mimi
nilikuwa juu ya daraja na wao walikuwa kwa chini. Kuonekana ndio
nilionekana kidogo ili kuweka maana ya wimbo kwa kuonekana vitendo
wafanyavyo watoto wa mtaani ambao ni yatima"
Post a Comment