Mfahamu Dogo Tundu aliyemdiss Dogo Janja kwa kumwambia anaiga ushoga


Dogo Janja ana mpinzani mpya. Bahati mbaya ama nzuri sio member wa Tip Top Connection. Anaitwa Dogo Tundu wa Arusha. Amini usiamini, dogo ni mkali balaa. Huenda ni maarufu jijini Arusha lakini kwenye cypher hii ya Wanene huenda akatambulika rasmi nchini. 

Kwenye cypher hii, wakubwa wamemwacha amalize verse ya mwisho na kuonesha ujuzi mkubwa kwenye punch na mashairi makali kama:

“Naitwa Dogo Tundu, rap sio mzungu, usiniletee kiwingu, nitakupiga manundu
Mimi ni kirusi nipo fast, kasi kama risasi kwenye beat nawapiga nazidi kukunja ngita,na siwezi kucheka hili life nimeteseka, machizi wameweka ngita kamanda bado napita mbuga nachapa kama mjeda, nimesimama imara kama Slaa wa Chadema.”
Lakini Dogo Tundu hakuishia hapo akaamua kumchana Dogo Janja:

“Nimezaliwa R, sijazaliwa Dar, mimi sio mshamba kama Janjaro wa Dar
Hakuna Dogo Janja, wala Dogo Jinga , yeye ni sharobaro na mimi ni mniga
Akitema Kirangi mimi nachana hadi Kichaga
Anaiga ushoga eti yeye ndo sharobaro.”

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates